logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond amdhalilisha Alikiba, amuita Malkia hadharani

Halafu Malkia katu yangu na wewe nani ana roho ya kusaidia watu? - Diamond aliuliza Kiba

image
na

Habari31 July 2023 - 05:05

Muhtasari


• Zuchu ni juzi tu amejiunga na Wasafi, Diamond alidai kuwa amempiku Alikiba katika muziki na wengine wengi waliostawi chini yake.

Diamond na Alikiba kwenye purukushani za mitandaoni

Msanii wa nyimbo za bongofleva nchini Tanzania Diamond Platnumz maarufu Simba amemtukana na kumdhalilisha mwenzake Alikiba hadharani katika mitandao ya kijamii kutokana na mzozo baina yao.

Diamond alitoa matamshi hayo katika mtandao wake wa Instagram, ambapo alimpiga vijembe Alikiba kwa kusema kuwa hakuna mwanamuziki hata mmoja aliwahi kunawiri chini ya ukufunzi wake Kiba.

Halafu Malkia unazungumzia roho ya kufukuta...kweli?...jamani hivi kati ya mie na wewe nani hana roho ya kusaidia watu? Wakati wewe tu mdogo wako wa damu umeshindwa kumsaidia anawiri kimuziki wakati ana uwezo mkubwa!” Alidakia Simba katika mtandao wake wa Twitter akimrejelea Alikiba.

Simba waaidha aliendelea kueleza na kukiri kwamba yeye huwa na roho nzuri ya kuweza kunawirisha wanamuziki wanaojihisi kustawi katika sanaa hiyo ambapo alitoa mfano wa binti aliyejiunga na Wasafi hivi karibuni Zuchu.

Halafu mie angalia watu ambao nilijitolea kuwanyanyua katika Muziki hadi wewe mwenyewe wakakupita. Mfano mzuri, Zuchu juzi tu kakuadabisha na Honey halafu sasa jiangalie na ujilinganishe na mie nani ana roho ya kusaidia watu katika muziki.” Aliendelea.

Alikiba maarufu Kingkiba waaidha alijibu shambulizi hilo katika mtandao wake wa Twitter kuwa anapaswa kuzoea kuhusu ngoma kali na kudai kuwa roho yake Diamond itamtia mawazo wengi hadi kufikia kujiunga naye.

Sema kwevo mdhaifu sana, tu-party tuwili tutatu na marafiki, interviews kadhaa na XXL, roho inakufukutaa, kutwa insta story...halafu inabidi uzoee kuhusu ngoma mfululu (kali),” Kiba akimjibu mwenzake katika purukushani zao za mitandao.

Haya yanajiri wakati ambapo utafiti wa Charts nchini Tanzania ulionesha kuwa nyimbo za Diomond Platnumz ndizo ziliongoza kuwa na watazamaji wengi katika YouTube, kwenye kipindi cha mwezi Juni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved