logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kimani Ichungwa kuongoza kikosi cha Kenya Kwanza kwa mazungumzo na Azimio

KK ina Kimani Ichung'wah, Aaron Cheruiyot Cecile Mbaririe, Hassan Omar na Catherine Wambilinga.

image
na Radio Jambo

Michezo02 August 2023 - 13:15

Muhtasari


• Kenya Kwanza ilisisitiza kuwa ghasia hazitakuwa tena na hazitakuwa sehemu ya mazungumzo ya kisiasa ya Kenya.

Ruto na Raila waonesha nia ya kupatana.

Muungano wa Kenya Kwanza umetaja wanachama wake watano ambao watauwakilisha katika mazungumzo mapya yaliyopendekezwa na upande wa Upinzani.

 Kikosi cha Kenya kwanza kitaongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung'wah, na wanachama wengine wakiwa Aaron Cheruiyot (Kiongozi wa Wengi katika Seneti), Gavana wa Embu Cecile Mbaririe, Hassan Omar (Mbunge wa EALA) na mwakilishi wa kike wa Bungoma Catherine Wambilinga. 

Kikosi cha Kenya Kwanza kinatarajiwa kuungana na wenzao wa Azimio wakiongozwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka pamoja na kiongozi wa Wachache Opiyo Wandayi, Eugene Wamalwa ambaye ni kinara wa DAP, Okong'o Omogeni na Mbunge wa Malindi Amina Mnyanzi. Kenya Kwanza katika taarifa siku ya Jumatano ilisisitiza kuwa watajadiliana na wenzao wa Azimio kuhusu masuala matano. 

Maswala waliotajwa ni pamoja na kuundwa upya kwa tume ya IEBC; utekelezaji wa kanuni ya kijinsia ya theluthi mbili, uboreshaji wa hazina ya maendeleo ya maeneo bunge, kubuniwa kwa Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani na Ofisi ya Mkuu wa Mawaziri. 

Katika taarifa yake Kenya Kwanza ilisisitiza kuwa ghasia hazitakuwa tena na hazitakuwa sehemu ya mazungumzo ya kisiasa ya Kenya.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved