Mama wa taifa Rachel Ruto amemuomboleza binamu yake ambaye alikumbuka kwamba ndiye aliyemkaribisha Nairobi kwa mara ya kwanza miaka kadhaa iliyopita.
Mama Rachel alisema kwamba binamu yake Sally Jepkemboi Mibey alikuwa mtu mzuri ambaye alimpokea Nairobi kwa mikono miwili na kumfanya kuhisi kama yuko nyumbani mbali na nyumbani.
“Sally Jepkemboi Mibey alikuwa zaidi ya binamu kwangu. Alikuwa dada, rafiki na mfano wa kuigwa. Alikuwa na roho ya kung'aa ambayo iligusa maisha ya wengi kwa upendo wake, wema na ukarimu. Alikaribisha kila mtu nyumbani kwake kwa uchangamfu na ukarimu.”
“Sitasahau mara ya kwanza nilipowasili Nairobi na jinsi alivyonikaribisha kwa mikono miwili. Alinifanya nihisi kama mimi ni sehemu ya familia yake. Alikuwa mwenyeji mwenye neema ambaye aliwafurahisha wageni wake kwa chakula kitamu, chenye lishe na kufariji,” mama Rachel alisema.
Mama Rachel alipakia picha ya jinsi hafla ya mwisho ya Sally ilivyokuwa na kusema kwamba siku zote ataishi kukumbuka fadhila zake.
“Alikuwa mama na mfano wa kuigwa kwa wengi. Hekima na imani yake iliwatia moyo wengi, na alinifundisha jinsi ya kuishi kwa neema na ujasiri. Imani yake ilikuwa ni nanga ambayo ilimpa nguvu na amani. Anaacha urithi wa upendo ambao utaendelea kuishi katika mioyo ya wale waliomjua. Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia. Pumzika kwa amani Sally.”