logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Picha za uchi: Mwanaume aliyechapisha picha za utupu za mpenzi wa zamani kulipa dola bilioni 1.2

Alimshutumu mpenzi huyo wa zamani kwa kuchapisha picha zake za ngono kwenye mtandao.

image
na Radio Jambo

Habari17 August 2023 - 05:33

Muhtasari


• Mawakili wa mwanamke huyo walidai kuwa mpenzi wake wa zamani alichapisha picha hizo ili kumtusi na kumdhalilisha machoni pa ulimwengu.

Mahakama ya jimbo la Texas nchini Marekani imemuamuru mwanaume mmoja kumlipa mpenzi wake wa zamani faini ya dola bilioni 1.2, baada ya kuchapisha picha zake za utupu kwenye mtandao.

Mwanamke huyo, alimshtaki mpenzi wake wa zamani kwa unyanyasaji wa kijinsia mnamo 2022.

Alimshutumu mpenzi huyo wa zamani kwa kuchapisha picha zake za ngono kwenye mtandao, baada ya wao kuachana, ili tu kumuaibisha kama kulipiza kisasi.

Mawakili wa mwanamke huyo walisema kuwa hukumu hiyo ni ushindi kwa yule wanayemtetea.

"Tumefurahishwa sana na uamuzi huo, kwa sababu utamwondolea unyanyasaji aliomfanyia", alisema Bradford Gilde, wakili mkuu wa mlalamikaji katika taarifa.

Awali, mawakili wake walidai mahakama imlazimishe mwanaume huyo kulipa faini ya dola milioni 100.

"Tunatumai kwamba faini hii itakuwa onyo kwa wale wanaofanya kama yeye, na kutoa somo kwa wale ambao wana tabia mbaya," alisema Bw. Gilde.

Mpenzi huyo wa zamani alishtakiwa kwa kutuma marafiki na jamaa zake anuani ya ukurasa uliochapisha picha hizo, ili waweze kutazama picha hizo.

Pia alishutumiwa kwa kuvamia mitandao yake ya kijamii na barua pepe yake, ili kumpeleleza.

Pia mpenzi wake wa zamani alishutumiwa kwa kumtumia ujumbe unaosema “Nina uhakika utakatisha maisha yako, unajaribu bila mafanikio kurudisha heshima yako ambayo imepotea kwenye mtandao. Kila mtu unayekutana naye atakutazama na kovu hili. Nakupongeza kwa kuingia katika uwanja huu wa mapambano.

Mawakili wa mwanamke huyo walidai kuwa mpenzi wake wa zamani alichapisha picha hizo ili kumtusi na kumdhalilisha machoni pa ulimwengu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved