logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mzee kijana: Akiwa na miaka 38 CR7 bado ni wa moto, amrambisha zulia beki - video

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or aliuvutia umati kwa kuonyesha ustadi wa kupiga hatua.

image
na Radio Jambo

Habari19 August 2023 - 07:52

Muhtasari


• Ronaldo alipitia kwa urahisi mabeki na kutia saini yake, na kuwaacha wakiwa wanyonge na kuhangaika kuendelea.

• Mchezaji huyo ameuanza msimu wake wa pili katika ligi hiyo kwa moto, japo timu yake ya Al Nassr imeshindwa kupata ushindi katika mechi mbili za ufunguzi.

Ronaldo.

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Christino Ronaldo maarufu kama CR7 bado ni wa moto licha ya umri wake kusonga Zaidi katika malimwengu ya soka.

Video ambayo imezua gumzo pevu mitandaoni inamuonesha nguli huyo wa chenga za kimaudhi akimambisha sakafu beki wa timu pinzani na kumuacha hoi taabani katika mechi ya pili ya ligi ya Saudi Arabia.

Sports Brief Kenya wanaripoti kwamba Nyota huyo wa Ureno amedumisha harakati zake za haraka na kuonyesha faini yake ya kipekee katika mchezo wa Al-Nassr wa Saudi Pro League Ijumaa jioni.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or aliuvutia umati kwa kuonyesha ustadi wa kupiga hatua juu chini dhidi ya Al Taawoun.

Ronaldo alipitia kwa urahisi mabeki na kutia saini yake, na kuwaacha wakiwa wanyonge na kuhangaika kuendelea.

Gwiji huyo wa Real Madrid kisha akapiga shuti lililowekwa wazi, ambalo lilipokelewa kwa jibu la haraka kutoka kwa kipa, ambaye aliokoa hatari kubwa kukataa jaribio la Ronaldo.

Mchezaji huyo ameuanza msimu wake wa pili katika ligi hiyo kwa moto, japo timu yake ya Al Nassr imeshindwa kupata ushindi katika mechi mbili za ufunguzi.

Ikumbukwe CR7 aliisaidia timu yake kushinda taji la ubingwa wa ukanda wa Uarabuni kwa mara ya kwanza katika historia yake, alipofunga mabao mawili ya ushindi dhidi ya Al Hilal wiki mbili zilizopita.

Hii hapa video ya chenga hizo za kimaudhi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved