Mjasirimali na mwanahabari Betty Kyallo amemnakilia dada yake Mercy Kyallo ujumbe maalum anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Alitumia Instagram yake kumsherehekea kwa picha za matukio yao mazuri wakiwa pamoja zikiambatana na ujumbe mfupi na mtamu wa siku ya kuzaliwa.
"Ni siku ya Mercy Kyallo duniani, heri ya siku ya kuzaliwa sis tuna furaha zaidi na mapambano makubwa zaidi tuna nguvu tunapokuwa pamoja. Wewe ni mshirika wangu pia, nakuombea tamaa zako za moyo wako zitimie kila wakati. afya njema, furaha na mafanikio na kila lililo jema likufikie. Nakupenda kila wakati," alinukuu.
Anatoka katika familia ya dada watatu na wana uhusiano mkubwa na pia wamefanikiwa mengi pamoja.
Watatu hao wana mfululizo wa filamu uitwao Kyallo Kulture ambao unahusu maisha yao kama dada.
Uhusiano mzuri wa dada hao umekuwa ukivutia wanamitandao pamoja na mashabiki wao.
Wanamitandao walimsaidia Betty kumsherehekea Mercy na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;
mounting: Happy birthday π to Mercy
women leadership: Amazing trailblazers of baby girls ππ
missmajor: Happy birthday to her. I wish I had sisters. You guys are rocking it.
stesh: It was a beautiful Series. Watched to the end. Is there a continuation coming up?
shedadinah: Ata sijaanza season oneπ’π’ mtu anilipie showmax tafadhali am missing out
emma: My twinnie happy birthday to he