logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Alinishika red handed!" Jamaa aachwa baada ya kufumaniwa na mpango wa kando

Dennis aliweka wazi kuwa anafahamu mpenziwe huyo bado amemngoja kwani bado hajaolewa na anasema atarudi.

image
na Radio Jambo

Habari22 August 2023 - 05:21

Muhtasari


•Dennis alisema ndoa yake ilivunjika mwaka wa 2020 baada ya mkewe kumfumania na mpango wa kando na kumuacha.

•Pauline alipopigiwa sumu, alikana kukosana na jamaa huyo na kudai kuwa alikuwa anasubiri ajipange ili waishi pamoja.

Ghost na Gidi

Jamaa aliyejitambulisha kama Dennis Natembea ,28, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Pauline Nanzala ,20, ambaye alimuacha takribani miaka mitatu iliyopita.

Dennis alisema ndoa yake ilivunjika mwaka wa 2020 baada ya mkewe kumfumania na mpango wa kando na kumuacha.

"Shida ilikuwa bi mambo na mpango wa kando. Unajua wanaume huwezi kuwa na mtu mmoja, alinishika red handed," Dennis alisimulia.

Aliendelea, "Nilikuwa nimeleta kamtu alafu bahati mbaya akanishika. Tulikuwa kwa nyumba yangu, alikuja akatupata. Alikasirika akaenda kwao. Nilitafuta mwingine kwani yeye alikuwa ameenda kwao kidogo. Nilimtafuta anasema atarudi lakini harudi. Alinipatia muda nibadilike na mimi nimebadilika "

Dennis aliweka wazi kuwa anafahamu mpenziwe huyo bado amemngoja kwani bado hajaolewa na anasema atarudi.

"Ameningoja, najua bado hajaoleka. Huwa ananiambia tu atarudi," alisema.

Pauline alipopigiwa sumu, alikana kukosana na jamaa huyo na kudai kuwa alikuwa anasubiri ajipange ili waishi pamoja.

"Apana, hatujakosana na yeye. Mimi nilienda tu kazi. Alikuwa shule na alisema nimngonje. Mimi nilimngoja ajipange. Ningekuwa nimekasirika ningekuwa nimepata  mtu mwingine. Mimi namngoja mpaka vile ataniambia," Pauline alisema.

Dennis hata hivyo alilalamika kuwa mpenzi huyo wake amekuwa akiahidi kurudi ila hajawahi kutimiza hilo.

Aidha, alimtaka mzazi huyo mwenzake kurudi mara moja ili waanze kuishi pamoja.

"Akuje saa hii.. Mimi nakupenda. Rudi tukae pamoja kama bibi na bwana. Nakupenda kama sweetpotato," alisema.

Pauline alisema, "Akiwa tayari ni sawa.. Baba Angel mimi nakupenda na roho yangu yote. Nilikuwa nangoja wakati utaniambia kama uko tayari nikuje. Sasa ni sawa."

Je, una ushauri gani kwa wawili hao?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved