logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Millicent Omanga alia ugani Emirates akishuhudia timu yake Man Utd ikititigwa na Arsenal

Arsenal waliichapa United mabao 2 kwa 1.

image
na Radio Jambo

Habari04 September 2023 - 05:00

Muhtasari


• Omanga alipakia picha za tikiti ya kuitizama mechi hiyo ugani Emirates pamoja na msururu wa picha akwia miogoni mwa mashabiki wengi.

Millicent Omanga

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha uwakilishi wa kike Nairobi ambaye pia aliteuliwa kama waziri msaidizi katika wizara ya usalama wa ndani Millicent Omanga ni mmoja wa Wakenya wachache waliobahatika kushuhudia ngarambe ya Manchester United na Arsenal ugani Emirates Jumapili alasiri.

Omanga ambaye ni shabiki mkuu wa United alianza mapema kutoa tambo zake dhidi ya mahasidi wao wa tangu jadi Arsenal akisema kuwa japo Arsenal walikuwa nyumbani, ilikuwa ni lazima kwao kusalimu amri baada ya United kukosa adabu za mgeni na kumuadhibu mwana Arsenal mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.

“Arsenali leo mambo ni matatu…MPIGWE, MCHAPWE AMA MLIMWE,” Omanga alijipiga kifua mapema kabla ya mechi.

Omanga alidokeza kwamba ni sharti angeshuhudia ngarambe hiyo moja kwa moja na hata kuoneshana tikiti za mechi hiyo kali akisema kwamba kwa ubora wa mechi hiyo, asingehubutu kukosa kuishuhudia.

Lakini baada ya mechi hiyo ambayo ilikamilika kwa Arsenal kuvuna ushindi mnono dakika za zima taa tulale, Omanga alijawa na hamaki huku akionesha kutofurahishwa kwake na jinsi timu yake ilivyopoteza udhibiti wa mechi na kuachia sare dakika za mwisho.

“Manchester United bora zaidi imecheza msimu huu mpya! Kushindwa kwa uchungu,” Omanga aliandika kauli ya kujiliwaza.

Arsenal walipata ushindi wa mabao 3 kwa 1 ambapo mabao mawili ya ushindi yalifungwa dakika za ziada.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved