logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Joeboy akiri kuwa na mimea 4 ndani ya nyumba yake ambayo anaongea nayo kila siku!

"Nadhani ni bora kuzungumza na mimea wakati mwingine kuliko kuzungumza na wanadamu"

image
na Radio Jambo

Habari05 September 2023 - 09:30

Muhtasari


• “Unahitaji utegemezo wa kiroho. Ni muhimu sana sana. Ikiwa hufanyi jazz [uchawi], lazima uombe," alisema.

Joeboy

Msanii wa Nigeria Joeboy kwa mara ya kwanza amefichua kuhusu ufanisi mkubwa wa taaluma yake kimuziki.

Joeboy ambaye alikuwa anazungumza kwenye podikasti moja iitwayo Zero Conditions alifichua kwamba ndani ya nyumba yake, ana mimea kama minne hivi ambayo anazungumza nayo.

Msanii huyo alimshangaza muongozaji wa podikasti hiyo aliposema kwamba kwake anaona wakati mwingine ni sahihi kufanya mazungumzo na mimea kuliko binadamu.

Joeboy alisema kwamba ndio maana amechora tattoo za mimea kwenye mwili wake, na kufichua kwamba mimea iliyopo kwenye sebule yake yote ameipa majina ya kibinadamu ambapo mara kwa mara yeye hufanya mazungumzo nayo.

"Binafsi, napenda asili. Ninapenda mimea. Nina mimea kama minne kwenye chumba changu. Niliiita Anthony, Themal, Raphael na Vanessa. Na kwa kweli ninazungumza nayo. Ninaiambia tu jinsi ninavyohisi. Nadhani ni bora kuzungumza na mimea wakati mwingine kuliko kuzungumza na wanadamu, " alisema mkali huyo wa Sip.

Joeboy alisema kwamba tofauti na watu wengine wanaoamini kaitka vitu vingine, yeye anaamini sana katika mimea, akitetea hali hiyo kwamba mtu yeyote ni lazima tu awe na asili ya kiroho – iwe ni ya Kimungu au Kichawi.

“Unahitaji utegemezo wa kiroho. Ni muhimu sana sana. Ikiwa hufanyi jazz [uchawi], lazima uombe," alisema.

Joeboy ni mmoja wa wasanii ambao wamefanikiwa kudumu kwenye tasnia ya muziki wa Afrobeats wenye ushindani mkali na mamia ya wasanii wenye vipaji vya aina yake wakitoka kila mwaka.

Lakini yeye amefanikiwa kushikilia nafasi yake kwa mashabiki wake, huku wasanii wengi wakija na kutoweka baada ya ngoma chache.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved