logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa afungulia mrembo wake duka la kuuza nguo, mrembo aolewa na mteja wa kiume

Sasa, amerudi juu vizuri zaidi kuliko alivyokuwa na msichana huyo amerudi tena

image
na Radio Jambo

Habari06 September 2023 - 12:31

Muhtasari


• Wizarab anaeleza kuwa mpenzi wa mwanaume huyo amerudi kwake baada ya kumlaghai mteja ambaye sasa ana uhusiano naye.

• Kulingana na chapisho lililoonekana, mwanamume huyo alitumia pesa kumtengenezea mpenzi wake boutique ili kujikimu kimaisha.

Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi

Hadithi moja ya mwanamke aliyemuacha mpenzi wake baada ya kufilisika imezua maoni kinzani katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter.

Hadithi hiyo iliyopakiwa na mtumizi mmoja wa mtandao huo kwa jina Sir Dickson ilisema kwamba jamaa huyo alimfungulia mpenzi wake biashara ya duka la kuuza nguo.

Baada ya jamaa huyo kufilisika, mrembo huyo alianza kumuona mpenzi wake kama kinyaa na badala yake akamtema na kuanza kuchumbiana na jamaa mwingine ambaye alikuwa mteja wa kununua nguo katika duka lake.

Kulingana na chapisho lililoonekana, mwanamume huyo alitumia pesa kumtengenezea mpenzi wake boutique ili kujikimu kimaisha.

Wizarab anaeleza kuwa mpenzi wa mwanaume huyo amerudi kwake baada ya kumlaghai mteja ambaye sasa ana uhusiano naye.

“Jamaa alifungua boutique kwa ajili ya mpenzi wake na alianza kuchumbiana na mteja wake kwa sababu alifilisika. Sasa, amerudi juu vizuri zaidi kuliko alivyokuwa na msichana huyo amerudi tena kutoka kimapenzi mteja wake,” alieleza jamaa huyo.

Jamaa huyo baada ya kurudiana mwanamke huyo alianza kumtumia mrembo wake vibaya huku akimshauri kula vyakula ambavyo nia yake ni kumharibu mwili wake.

Hili, alisema kuwa alilifanya kimakusudi kama njia moja ya kulipa kisasi kwa mrembo huyo kwa kumfanyia mabaya siku za nyuma.

“Amemgeuza kuwa mtumwa wa ngono na kumfanya achukue vitu vyenye madhara ili kumwangamiza,” aliongeza.

"Alisema ana huzuni na amekufa ndani lakini bado hajamalizana naye. Anataka kummaliza kabisa. Hatumii pesa kwa ajili yake isipokuwa anapata kitu cha kumdhuru, kwa sababu yeye si mpenzi tena. Watu wanalipiza kisasi. Moyo wa binadamu 🤷‍♂️" alimaliza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved