logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Caicedo wa Chelsea amrambisha Messi sakafu kwenye Argentina vs Ecuador - video

Mechi hiyo iliisha kwa Argetnina kushinda bao 1-0 kwa hisani ya mkwaju wa mpira mfu wa Messi.

image
na Radio Jambo

Habari08 September 2023 - 10:17

Muhtasari


• Alikuwa mzuri sana hivi kwamba mshindi huyo wa Ballon d'Or mara saba, wakati mmoja, alitambua kwamba alikuwa akipambana na kiungo sahihi.

Messi akihangaishwa na Caicedo katika mechi ya Ecuador vs Argentina.

Moises Caicedo, kiungo wa kati wa Chelsea ambaye aliingia kwenye vitabu kama mchezaji ghali Zaidi kuwahi kununuliwa nchini Uingereza mwezi uliopita na Chelsea akitokea Brighton ameonesha ni kwa nini anastahili.

Japo mchezaji huyo katika mechi mbili ambazo amecheza ndani ya uzi wa Chelsea hajaonesha viwango vya kuthibitisha bei yake ya juu, katika mechi ya kulitumikia taifa lake, Caicedo alionesha ubora wake mbele ya mchezaji nambari moja duniani kwa muda wote, Lionel Messi.

Vikwazo, maadili ya kazi, nguvu, uchezaji wa pasi, na stamina ndivyo kocha yeyote angetaka katika kiungo mkabaji - Mkukwado huyo ana sifa nyingi zaidi, kama si zote, kati ya hizi Sports Brief wameripoti.

Ikiwa video inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni kitu cha kupita, nyota huyo wa Chelsea alivutia kwani alifanikiwa kumpokonya mpira nyota wa kipindi hicho, Lionel Messi, mara kadhaa.

Alikuwa mzuri sana hivi kwamba mshindi huyo wa Ballon d'Or mara saba, wakati mmoja, alitambua kwamba alikuwa akipambana na kiungo sahihi.

Messi alionyesha heshima yake kwa kunyoosha mikono yake ili kumrudisha Caicedo kwenye miguu yake katika ishara ya kweli ya uchezaji.

Katika mipira yote kumi ambayo ilimkutanisha Caicedo na Messi kwenye kiungo cha kati, Caicedo alifanikiwa kumpokonya Messi mpira mara nane kati ya hiyo kumi.

Tazama video hapa chini;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved