logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati, Diana watofautiana vikali na pasta Ezekiel baada ya kudai kina Diana sio wa kuolewa

Katika majibu yake kuhusu matamshi ya mchungaji huyo, Bahati alisema kuwa kina Diana ndio bora zaidi.

image
na Radio Jambo

Habari11 September 2023 - 19:46

Muhtasari


•Bahati na mke wake Diana Marua wametofautiana na mhubiri maarufu Ezekiel Odero kuhusu matokeo mabaya ya kuoa wanawake wanaoitwa ‘Diana’.

•Katika majibu yake kuhusu matamshi ya mchungaji huyo, Bahati alisema kuwa kina Diana ndio bora zaidi.

Mwimbaji wa Kenya Kelvin Kioko almaarufu Bahati na mke wake Diana Marua wametofautiana na mhubiri maarufu Ezekiel Odero kuhusu matokeo mabaya ya kuoa wanawake wanaoitwa ‘Diana’.

Video ya mchungaji huyo mashuhuri akitaja sababu kadhaa za kwa nini wanaume wanapaswa kuwaepuka kina Diana ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua mjadala mkubwa nchini kote.

Kweli, video hiyo iliwafikia wanandoa hao maarufu na kuwachochea majibu ambapo walitofautiana naye na kumbainishia kuwa wamekuwa kwenye ndoa thabiti kwa takriban miaka 7. Katika majibu yake kuhusu matamshi ya mchungaji huyo, Bahati alisema kuwa kina Diana ndio bora zaidi.

“Huyu ni Nabii WA KWELI au WA UONGO??? Mtu mwambie Mchungaji huyu Aache Kupotosha Kanisa. @Diana_Marua nami tunasherehekea Miaka 7 ya Ndoa Ijayo OKTOBA, TAREHE 20. DIANAS NDIO BORA!!!” Bahati alisema.

Akijibu video hiyo hiyo, Diana Marua aliwaonya wanawake dhidi ya kuolewa na wanaume ambao wanaitwa Ezekiel huku akiwataja kuwa ‘waongo’.

“Usiolewe na Ezekiel!!! Watakutazama moja kwa moja machoni pako na UONGO! Je, huyu ndiye Ezekieli aliyekuwa sehemu ya MAUAJI YA SHAKAHOLA????” Diana alisema.

Katika kanda ya video ambayo imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, mchungaji Ezekiel Odero alianza kwa kuwauliza waumini wake kama wamewahi kushuhudia mwanamke yeyote mwenye jina Diana akiwa kwenye ndoa.

Ezekiel alisema kuwa iwapo mwanamke kwa jina Diana atafanikiwa kuwa kwenye ndoa, basi ndoa hiyo moja kwa moja huwa inaongozwa na yeye huku mwanamume akilazimika kufuata masharti yake kama ambavyo maji yanafuata mkondo.

“Umeshawahi kuona Diana yeyote kwa ndoa? Hakuna hata mmoja hivi. Ukioa Diana uishi na yeye, yeye ndiye anakuongoza kama robot anakubeba hivi, utaishi na Diana, anakuwa mwanamume. Lakini wewe uwe mume, Diana anaenda. Hapo nimeongea ukweli,” Pasta Ezekiel alisema.

Jambo la pili ambalo aliwashauri waumini wake ni kukoma kuwapa wanao majina ya Diana akisema ni majina yenye historia isiyo nyooka.

“Usimpe mtoto wako jina Diana, sababu akiolewa, utamshare na watu, Diana anapendwa bila sababu hata kama hajui. Bila yeye kujua, mtu anamwambia nikikwangalia akili inachanganyikiwa, kwa sababu jina hilo linabeba roho mbaya,” Ezekiel alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved