logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Anapendwa Kenya sana!, Eric Omondi amemlaki mwimbaji Chritina Shusho

Shusho yuko Kenya kwa mwaliko wa Eric Omondi.

image
na

Habari14 September 2023 - 09:48

Muhtasari


•Shusho alichukua nafasi hiyo kwenye mazungumzo na kuwasifia waimbaji wa nyimbo za muziki wa Kenya na kusema kwamba wanafanya vyema japo anahisi kuwa kuna mapungufu.

 

Mwigizaji na mcheshi maarufu wa Kenya na Afrika Mashariki Eric Omondi amemlaki mwimbaji wa nyimbo za injili wa Tanzania  Chritina Shusho.

Hii ni baada ya shusho kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA kwa mwaliko wa Eric Omondi  ambaye alitoa hakikisha la kurejesha muziki wa injili ambao anadhani kwamba unadidimia.

Akizungumza, Eric alidai kuwa anahisi muziki wa injili wa kenya unadidimia na hivyo atafanya kila juhudi kuulainisha.

'Mimi binafsi kama Eric, nahisi kwamba kuna wakati kama Kenya tulikua na uamsho, na nahisi kwamba tunaitaji kumrejelea Mungu. Na nilipongalia nikaona kwamba Shusho ndiye mwimbaji pekee aliy na wito kutoka kwa Mungu na anaweza kutusaidia kumrejelea Mungu."

Shusho alichukua nafasi hiyo kwenye mazungumzo na kuwasifia waimbaji wa nyimbo za muziki wa Kenya na kusema kwamba wanafanya vyema japo anahisi kuwa kuna mapungufu.

Shusho Alimsifia mwimbaji, Mercy Masika, Daddy Owen na Gardian Angel na kusema kazi yao ya uimbaji wa nyimbo za injili inafanya vyema.

Kwa matani Eric Omondi alimkosoa Shusho na kusema kuwa kwa sasa mwimbaji ambaye ni tajika ni Mercy masika.

Shusho alisema kuwa uimbaji wa nyimbo za injili unahitaji kumjua Mungu zaidi na kujikubali kuwa wewe kwa kupata neema ya Mungu bali si kufanya mambo ambayo hayaambatani na maudhui ya kimungu.

'Hata kama una roho kubwa namna gani lazima ujue kuwa wewe ni mwanadamu na una mapungufu, ukiwa na shida sma watu wakusidie, usije ukasema kila kiutu wewe uko sawa kwa kufeki,"

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved