logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwili wa mvuvi wapatikana siku 10 baada ya kuzama majini

Moja  kati ya mili ya wavuvi waliozama maji wapatikana

image
na

Habari18 September 2023 - 11:11

Muhtasari


•Baada ya juhudi za wavuvi katika ziwa victoria wamefanikiwa kutoa maiti ya mmoja wa wavuvi na ambaye alizama maji

Wavuvi katika Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Koginga huko Homa Bay Picha: MAKTABA.

Mwili wa mvuvi mwenye umri wa miaka 40 kutoka ufukwe wa kisiwa cha Remba kaunti ya Homa Bay, aliyekufa maji akivua samaki katika ziwa Victoria siku 10 zilizopita umepolewa. 

Mwili wa Daniel Otieno ulipatikana karibu na Kisiwa cha Migingo katika Kaunti ya Migori Jumapili jioni na kundi la wavuvi.

Otieno alikufa maji pamoja na mvuvi mwingine ambaye bado hajapatikana. Walikufa maji wiki mbili zilizopita walipokuwa kwenye shughuli za kuvua karibu na Kisiwa cha Migingo.

Kulingana na mwenyekiti wa Kitengo cha Usimamizi wa Ufuo Zemekiah Okoth Mamra, Otieno na Ochieng walikumbana na kifo chao kufuatia ajali iliyohusisha meli na mashua katika Ziwa Victoria.

Mashua ilivunjika vipande viwili, na kufanya sehemu moja ambayo wavuvi wawili walikuwa wameketi kuzama.

Mamra alisema wawili hao walikuwa miongoni mwa wavuvi waliokuwa wanaelekea kuvua samaki aina ya omena.

Wakati huo huo, shughuli ya kutafuta mwili wa Ochieng inaendelea. Kulingana na mila, ni kuwa watafanya juhudi zote wakisaindiana na wataalamu wenye ujuzi wa kuogelea ili kusaka mwili huo hadi upatikane.

Wavuvi wameombwa kuwa wangalifu wakati wanapoendesha kazi yao ya kuvua samaki katika ziwa na hata maeneo mengine yenye maji mengi .

Wengi wa wavuvu katika ziwa Victoria wanasema kuwa wanapitia changamoto nyingi wakati wanapoingia majini kwa ajili ya kuvua samaki.

Wavuvi hawa wameomba serekali kuwawezesha kupata vifaa ambazo wanaweza kutumia na ambavyo vitawasaidia wakati wa ajali majini. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved