logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+VIDEO) Harmonize aanguka jukwaani akimtumbuiza Rais Samia

Rais Samia alionekana akicheka wakati huo pamoja na watazamaji

image
na Radio Jambo

Habari18 September 2023 - 13:47

Muhtasari


  • Haijabainika kama anguko hilo lilikuwa sehemu ya uchezaji wake lakini aliinuka haraka na kuendelea na uchezaji wake.
Harmonize

Staa wa Bongo Fleva, Harmonize alikumbana na tukio la aibu alipokuwa akitumbuiza katika eneo la Ruangwa, Lindi wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu.

Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya Harmonize kutumbuiza wimbo wake maarufu Teacher.

Mwimbaji alikuwa ameanza kucheza, akionyesha dansi zake za kusisimua alipoanguka ghafla.

Haijabainika kama anguko hilo lilikuwa sehemu ya uchezaji wake lakini aliinuka haraka na kuendelea na uchezaji wake.

Rais Samia alionekana akicheka wakati huo pamoja na watazamaji

Hata hivyo Harmonize ametoa shukrani zake kwa rais Samia kwa kuwaunga mkono wasanii. Aidha aliapa kumuunga mkono mkuu wa nchi katika uongozi wake.

"Thank You Thank You my President πŸ™πŸ™ Ndani Yako Kuna Huruma Na Upendo!!!! Mkubwa Sanaa!!!! Natambua Na Kuthamini Heshima Hiii Uliyonipatia Mimi & Upendo wako Mkubwa Kwa Wasaniii Na Sanaa Kwa Ujumla πŸ™ Mungu Akutilie Wepesi Uendelee Kuzigusa Sekta Zote Muhimu Zenye Tija Katika Taifa Lako!!! Hili tukufu Tanzania !!!!! NIKUAHIDI TUU Yakwamba Tunasimama Na wewe Tunatamba Na Wewe!!! Full stop βœ‹ Mazungumzo Majadiliano TUKUTANE (2030),” aliandika msanii huyo.

Hii hapa video ya tukio hilo;

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved