Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 alifariki baada ya vita na mpenzi wake wa zamani kuhusu runinga katika kijiji kimoja kaunti ya Meru.
Mpenzi huyo wa zamani alimpiga mwanamke huyo kichwa baada ya kudaiwa kujaribu kuingia katika nyumba yake katika kijiji cha Muringambugi, polisi walisema.
Mwanaume huyo alidai marehemu alikwenda nyumbani kwake akiwa na jiwe na kuanza kutoa televisheni, mashine ya kuchomelea na mashine ya kusagia ili kuziuza.
Hili lilizua mzozo kati ya wawili hao ambao ulimwacha mwanamke huyo na majeraha mabaya kichwani.
Mwanamume huyo baadaye aliripoti kisa hicho kabla ya polisi kufika katika nyumba hiyo ambapo walimkuta mwanamke huyo akiwa na majeraha mabaya kichwani.
Mshukiwa alizuiliwa baada ya tukio hilo. Aliwaambia polisi kwamba walikuwa wametofautiana miezi iliyopita na mwanamke huyo alihama kutoka nyumbani walokoishi naye.
Polisi walisema viti viwili, jiwe, na kitambaa cheupe chenye madoa ya damu vilipatikana na kuwekwa kama vielelezo vya ushaindi kufuatia kifo cha mwanamke huyo.
Mwili wa mwanamke huo ulichukuliwa na polisi na kusafirishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi zaidi kufuatia kifo icho.
Polisi walisema mshukiwa anatarajiwa kortini ambapo walinuia kuomba siku zaidi ili kuwawezesha kukamilisha uchunguzi wao.
