logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ni dada Zangu-Nadia azungumza baada ya kuwaonyesha kivumbi Zuchu na Nandy

Amesema sio sifa zake kudhalilisha wanawake walio kwenye tasnia ya muziki

image
na

Habari28 September 2023 - 09:46

Muhtasari


•Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kimataifa JKIA,Nadia amesema kuwa msanii Zuchu na Nandy ni dada zake kimziki na hivyo anawatambua

Nadia mukami asema Zuchu na Nandy ni dada zake kimziki Picha Instagram

Msanii na mtunzi wa nyimbo Nadia Mukami amefunguka kuhusu uhusiano wake na wasanii tajika wa kike wa Tanzania Zuchu na Nandy.

Nadia  ambaye amerejea nchini baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya Afrika kitengo cha wanawake  Afrika Mashariki amaesema awezi akashusha heshima aliyonayo kwa wasanii maarufu aliowashinda kwenye mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kimataifa JKIA,Nadia amesema kuwa msanii Zuchu na Nandy ni dada zake kimziki na hivyo anawatambua.

Ameeleza kuwa hawezi akashusha heshima yake kwa sababu wanafanya kazi pamoja, akisema kwamba kuna ngoma ambayo wanaandaa yeye pamoja  na Nandy.

"Ni dada zangu,hasa Nandy kuna ngoma tunaandaa na yeye,kwa hiyo siwezi nikawadhalilisha dada zangu. Sio sifa zangu kudhalilisha wanawake walio kwenye tasnia ya muziki,muda mwingine ni  matani ya mitandaoni tu ila nawaheshimu." Alisema

Hivi majuzi,Nadia alidai kuwa yeye ni msanii tajiri Afrika Mashariki na kusema kwamba hakuna msanii wa kike Afrika Mashariki anamshinda kifedha.

Kutokana na kauli hii pamoja na  ushindi wake uliowabwaga mabingwa tajika kwenye tasnia hiyo ya muziki Afrika Mashariki, mashabiki walidhania kuwa Nadia angetema moto kwa wenzake,jambo ambalo alikanusha kwenye mazungumzo.

Nadia Mukami alirejea nchini baada ya ziara yake wiki mbili Marekani alikoenda kwa ajili ya sherehe ya tuzo za AFRIMMA.

Alisema kuwa si jambo la busara wasanii kudhalilishana ila ni muhimu wao kushirikiana kuhakikisha tasnia ya muziki Afrika inatamba.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved