logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nitaanza kutoa miziki aina ya Reggae - Jay Melody afichua

"Wimbo ukifanya vizuri ishaallah na usipofanya vizuri pia namshukuru Mungu " alisema.

image
na Radio Jambo

Habari28 September 2023 - 07:31

Muhtasari


• "Nyimbo zangu nyingi zinaanza hivyo kwa kasi ya mwendo pole lakini baadae huchukua kasi na kushika,” alikumbuka.

Jay Melody.

Mkali wa Bongo Fleva, Jay Melody amesema kwamba yeye hana mipaka katika kutoa miziki ya aina Fulani pekee, akikiri kwamba huwa anawasikiliza mashabiki wake na kuwapa kile ambacho wangependa kusikia kutoka kwake.

Melody ambaye alikuwa anazungumza na mwanablogu mmoja nchini Tanzania alizungumzia pia jinsi mashabiki wake walivyompokea kwa njia hasi alipotoa kibao chake cha kwanza chenye mtindo wa Amapiano.

“Mimi nashukuru kila hali, sio tu Amapiano nimetoa halafu haikufanya vizuri, labda watu wakaona nimeswitch sana. Lakini wakati mwingine mashabiki wanatupenda wakiona tunafanya muziki ule ule, lakini wakituona tunaendelea vile vile pia wanatuhama na kutafuta msanii mpya. Ndio maana ni vizuri kwa msanii wakati mwingine unafaa kuwaza mashabiki wana masikio gani,” alisema.

Msanii huyo alifichua kwamba yeye hatokuwa na mipaka katika miziki ambayo anataka kuitoa mradi imetakwa na mashabiki wake, akifichua kwamba yuko radhi kuanza kutoa hata miziki yenye midundo ya Reggae.

“Kila hali mimi naipokea kutoka kwa mashabiki – wale wanaonijibu hasi na wale wanaonijibu chanya. Wimbo ukifanya vizuri ishaallah na usipofanya vizuri pia namshukuru Mungu kwa sababu tunachokifanya si kwamba kitamfurahisha kila mtu au kikawa bora muda wote. Mimi nitaendelea kutoa tu ngoma zangu haijalishi. Hata Amapiano nitatoa, hata sijui Reggae nitatoa,” Melody alisema.

Msanii huyo alisema kwamba kwa kipindi ambacho amekuwa kwenye tasnia, amejifunza kukubali majibu ya aina zote, akikumbuka hata wakati anaota ngoa iliyompaisha ya ‘Nakupenda’ watu walimsuta sana lakini pindi muda ulivyozidi kusonga na mashabiki kupata ustahimilifu wa kusikiliza ngoma walikuja kuipenda.

“Nakumbuka hata kipindi natoa ‘Nakupenda’ watu walicharuka wakisema ngoma gani hii. Ngoma ya taratibu hiyo watu wanatoa Amapiano sasa hivi, lakini ikaja ikafanya vizuri. Nyimbo zangu nyingi zinaanza hivyo kwa kasi ya mwendo pole lakini baadae huchukua kasi na kushika,” alikumbuka.

Msanii huyo aliwapa maua mashabiki wake wa Kenya akisema kwamba kwa mapenzi wanayompa imemsababishia yeye kufanya shoo nyingi Kenya kuliko zile ambazo amefanya nyumbani Tanzania.

"Mimi nawapenda sana Wakenya kwa sababu hata ukiangalia Boomplay ya Kenya mimi nina ngoma 5 pale juu. Yaani ngoma kama Nakupenda ina miaka 2 lakini bado inafanya vizuri Kenya," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved