Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC) kwa mara nyingine imetangaza kukatizwa kwa umeme ambako kumepangwa kufanyika siku ya Ijumaa, Septemba 29.
Maeneo kadhaa katika kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Homa Bay na Kirinyaga.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Evergreen ikiwemo mtaa wa Runda Evergreen, Runda Meadows, Duom Palm Street, Tara Rd, Cactus Street, Baobab Street, Ebony Street, Garden Drive, Woodvale Drive, Flame Treem, Mugumo Drive, sehemu ya barabara ya Ruaka na viunga vyake zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Ndiwa na Sukari Industries katika kaunti ya Homa Bay zitaathirika na ukosefu wa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri. Miongoni mwa sehemu zitakazoathirika ni Mirogi Complex, Ruma National Park,Ongeng Market, Soko ya Ndiwa, Ojode Unga, Sukari Industries, shule ya msingi na ya upili ya Ligodho, Miranga Market, Kalamindi Market, Wachara Market, Kobama Market,Ratanga Market, Nyamogo Girls, Got Kojowi Market, Ranen Mikumi na viunga vyake.
Katika kaunti ya Kirinyaga, sehemu za maeneo ya Kutus mjini na Kithiririti zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri. Sehemu zitakazoathirika ni pamoja na Kutus mjini, Kutus sokoni, Delta Petrol station, Kithiririti, Kafathiro, Kiangai, Kiorugari sokoni na viunga vyake.