logo

NOW ON AIR

Listen in Live

[Picha] Kutana na mama mkwe wa Zari Hassan, mamake Shakib Lutaaya

Ni maelezo kidogo kuhusu familia ya mpenziwe Zari, historia yake na maisha ya kibinafsi yanajulikana.

image
na Radio Jambo

Habari01 October 2023 - 10:13

Muhtasari


•Shakib alimsherehekea mzazi huyo wake kwenye mtandao wa kijamii ambapo alichapisha picha zake na kuziambatanisha na emoji za moyo ambazo mara nyingi huashiria upendo.

•Shakib alizaliwa Kampala, Uganda mwezi Desemba 1992 na kukulia huko kabla ya kuhamia Afrika Kusini baadaye maishani kwa ajili ya kutafuta riziki.

Mume wa mwanasholaiti  na mfanyibiashara Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya kwa mara ya kwanza amemtambulisha mama yake mzazi kwa umma.

Siku ya Jumamosi, mfanyibiashara huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 31 alimsherehekea mzazi huyo wake kwenye mtandao wa kijamii ambapo alichapisha picha zake nzuri na kuziambatanisha na emoji za moyo ambazo mara nyingi huashiria upendo.

Shakib pia aliambatanisha picha hizo na sauti ya mwanaume anayesikika akituma ujumbe wa sifa kwa mama yake.

“Sio kosa lako Ma. Umelea mtoto mzuri sana. Ulimwengu uliniangamiza tu na kunigeuza kuwa mtu asiye na maana,” ilisema sauti hiyo ya mwanaume ambayo Shakib aliambatanisha na picha zake na za mama yake.

Chapisho la hivi punde  la mfanyibiashara huyo linaonyesha upendo mkubwa alionao kwa mzazi wake na uhusiano mzuri kati yao.

Tazama picha za mamake Shakib, mama mkwe wa Zari Hassan:

Shakib Lutaaya ,31, Shakib ni mchumba wa mwasosholaiti maarufu wa Uganda na mjasiriamali Zari Hassan ,43, na wawili hao wanatazamia kufunga ndoa rasmi hivi karibuni.

Barua ya mwaliko wa harusi iliyofikia Radio Jambo inaonyesha kuwa wanapanga kufanya harusi siku ya Jumanne, Oktoba 3 mwendo wa saa sita adhuhuri.

“Zarinah Hassan na Shakib Lutaaya wanakualika kwa moyo mkunjufu kushiriki katika furaha na kusherehekea siku yao ya harusi. Tarehe: 3 Oktoba 2023. Saa: 1200. Uwepo wako kwenye siku hii maalum utafanya sherehe yetu isisahaulike.” ilisomeka barua ya mwaliko iliyosainiwa na Zari na Shakib.

Hafla hiyo ya hrusi itakayofanyika nchini Afrika Kusini itahudhuriwa na wageni wachache ambao wamealikwa na maelezo mengi kuihusu ya kuwekwa faragha. Haijabainika kwanini wapendanao hao wameweka harusi yao kuwa siri kubwa.

Shakib alizaliwa Kampala, Uganda mwezi Desemba 1992 na kukulia huko kabla ya kuhamia Afrika Kusini baadaye maishani kwa ajili ya kutafuta riziki. Ni maelezo kidogo kuhusu familia yake, historia yake na maisha ya kibinafsi yanajulikana.

Zari Hassan pia alizaliwa nchini Uganda katika mji wa Jinja kwa wazazi wa Uganda  Nasur na Halima Hassan. Babu yake mzaa mama ni Mhindi ilhali nyanya yake anatoka Uganda, pengine sababu ya yeye kuwa na ngozi nyeupe kwa kiwango.

Wapenzi hao walikutana nchini Afrika Kusini miaka kadhaa iliyopita, wakachumbiana kwa muda kabla ya kutengana na baadaye kuungana tena mwaka jana. Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu katika harusi ya Kiislamu (Nikah) mwezi Aprili mwaka huu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved