logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke awaua 3 akiwemo mtoto wake wa miezi 3 Elgeyo Marakwet

Kulingana na walioshuhudia, mwanamke huyo alizinduka Jumapili usiku, akaokota panga,

image
na Radio Jambo

Habari02 October 2023 - 13:47

Muhtasari


  • Watu wawili zaidi walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo la usiku na kupelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi, ambapo wamelazwa kwa matibabu.
crime scene

Polisi huko Elgeyo Marakwet wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja aliwakatakata watu watatu hadi kufa, akiwemo mtoto wake wa miezi mitatu.

Kulingana na walioshuhudia, mwanamke huyo alizinduka Jumapili usiku, akaokota panga, na kuwashukia watu watatu eneo la Elgeyo Marakwet eneo la Katilit.

Watu wawili zaidi walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo la usiku na kupelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi, ambapo wamelazwa kwa matibabu.

Bado haijabainika sababu ya mauaji hayo, lakini polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu suala hilo.

Haya yanajiri miezi michache baada ya mwanamke mmoja Kitebngela kumkatakata na kumla mwanawe, baada ya kukosana na baba ya mtoto wake.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved