logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya kufunga vituo binafsi vya kulea Watoto kwa hofu ya biashara ya binadamu

Serikali ya Kenya imetangaza kufunga nyumba zote za watoto zinazomilikiwa na watu binafsi ndani ya miaka minane.

image
na Radio Jambo

Habari03 October 2023 - 03:50

Muhtasari


•Serikali ya Kenya imetangaza kufunga nyumba zote za watoto zinazomilikiwa na watu binafsi ndani ya miaka minane.

Kenya kuondoa nyumba za watoto za kibinafsi, Serikali ya Kenya imetangaza kufunga nyumba zote za watoto zinazomilikiwa na watu binafsi ndani ya miaka minane, ikisema hilo litasaidia kwa kiasi kukomesha ulanguzi wa watoto.

"Katika miaka minane ijayo nyumba za kibinafsi hazitakuwepo."

Tunahitaji kujiandaa ili kuwaweka katika mazingira mazuri watoto hao ambao watatoka katika nyumba za kibinafsi," Waziri wa Kazi na maendeleo ya Jamii Florence Bore alisema katika hafla siku ya Jumapili.

Bi Bore alikuwa amechapisha kwenye X (zamani Twitter) mapema Jumamosi kwamba serikali tayari ilikuwa katika harakati za kufunga nyumba za watoto na yatima.

Alisema watoto katika taasisi hizo watawekwa katika malezi ya familia na jamii, jambo ambalo alisema linatoa mazingira bora kwa watoto hao. Wenyeji wanasema kuna zaidi ya watoto 40,000 katika takriban nyumba 800 za kulea nchini Kenya.

Mengi ya haya yanafikiriwa kuendeshwa kibinafsi.

Kenya imekuwa ikitafuta kuondoa nyumba za kibinafsi za watoto na nyumba za watoto yatima tangu kupitishwa kwa Sheria ya Mtoto ya 2022, ambayo inataka mabadiliko ya ulezi, uwekaji wa malezi na kuasili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved