logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatuvalii kwa ajili ya wanaume - Kate Actress asema

Hatuvalii kwa ajili ya wanaume-Kate Actress asema

image
na

Habari09 October 2023 - 07:30

Muhtasari


• Katika kusherehekea mafanikio yake,Kate alitumia akaunti yake ya Insta kushiriki picha yake ya kupendeza,yenye umaridadi na haiba akiwa amevalia mavazi ambayo hayakuwa na ukamilifu.

• "Hatuvalii wanaume."

Kate Actress.

Mwigizaji Kate Actress,aliibuka mshindi katika Tuzo za kifahari za Pulse Influencer mwaka wa 2023,zilizoandaliwa Oktoba 8,katika ukumbi wa Nairobi Street Kitchen.

Mwigizaji huyo mashuhuri na mshawishi alitwaa Tuzo ya mwanamtindo bora .

Katika kusherehekea mafaninia yake,Kate alitumia akaunti yake ya Insta kushiriki picha yake ya kupendeza, yenye umaridadi na haiba akiwa amevalia mavazi ambayo hayakuwa na ukamilifu.

Picha hiyo ilipogusa mpasho wake,mashabiki wake waaminifu walimumiminia sifa za urembo wa kuvutia pamoja na jumbe za pongezi.

Hata hivyo,huku kukiwa na na wingi wa pongezi kutoka kwa mashabiki,shabiki mmoja mwenye shauku,anayetambulika kama mrlink752, aliibua swali ambalo Mwigizaji Kate alilazimika kujibu.

@mrlink752 aliwaza ni kwa nini mashabiki hao wa kiume hawakuwapo wakati wa pongezi.

"Asilimia 99 ya pongezi imetoka kwa wanawake, wanaume wako wapi?"Aliuliza.

Kate,alimjibu shabiki huyo kwa ujasiri akisema;

"Hatuvalii wanaume." Kate alimjibu.

Wiki kadhaa zilizopita,Kate aligonga vichwa vya habari kufuatia tangazo lake la kuachana na mumewe,Philip.

Uamuzi huu ambao ulivutia umakini mkubwa,ulionyesha azimio lake la kutanguliza furaha yake na safari ya kibinafsi.

Kate pamoja na mastaa wengine wengi waling'aa katika sherehe za Tuzo za mwaka huu za Pulse Influecer Award.

Marya Okoth alitawazwa kuwa mwigizaji Mshawishi wa Mwaka, Abel Mutua alitwaa tuzo ya Mshawishi Bora wa Mwaka kwa upande wa YouTube,huku Tom Daktari akiibuka kuwa Mshwishi Bora wa Mwaka upande wa TikTok.

Tuzo za Pulse Inlfuencer za mwaka huu hazikusherehekea tu mafanikio ya watu hawa mashuhuri bali pia zilisisitiza ushawishi unaokua wa waundaji wa maudhui ya kidijitali na uwezo wao wa kuchagiza mitindo na mitazamo katika ulimwengu wa kisasa unaoenda kasi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved