logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wema Sepetu afunguka na kusema vile maneno ya mamake bado yanamkata roho

Wema asimulia kukekwa jinsi mamake aliondoka kwenye sherehe yake bila kuagana

image
na

Habari12 October 2023 - 06:37

Muhtasari


• Nilichagua Furaha Fm kwa maana ni Radio ya vijana ambayo ndio bora zaidi kwangu nadhani nitapata ushauri ndiposa nirudie maisha yangu ya furaha ya awali.

 Muigizaji mashuhuri wa muda mrefu ambaye  kwa wakati mmoja alikuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu amekiri kuzama kwenye dimbwi la huzuni baada ya kuaibishwa hadharani na mama yake mzazi.

Kisa hicho kilitokea wakati wa sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Nyota huyu wa kuigiza amesimulia vile tabia za mamake zilimuathiri kisaikolojia ndiposa akajiunga ka kituo cha Furaha Fm nchini Tanzania ili kupata ushauri kutoka kwa wafuasi wake na wachungaji ili kupata mwelekeo wa maisha.

"Mimi na mamangu mzazi  Mariam Sepetu hatujakuwa vyema baada ya tafrija hiyo ambayo iligeuka kuwa kinyume nilivyotarajia, ndio maana naendelea kupata ushauri kutoka kwa jamii na watumishi wa Mungu kwa maana mimi ni kioo cha jamii na watu wengi wanaiga mfano wangu ndio maana napenda ushauri,"alisema Wema Sepetu.

Wema alipata ushauri kutoka kwa mchugaji mmoja kwenye kituo hicho ila alisema bado roho yake inatamani kupata zaidi hadi wakati ataporidhika na kurudia maisha yake ya awali.

"Mamangu  aliondoka kwa sherehe yangu bila kuagana, bali pia mpenzi   wangu Whozu naye aliondoka nyumbani akiwa amejawa na hasira, jambo ambalo linaniathiri sana kisaikolojia hadi kufikia hatua ya kutafuta faraja kwa pombe, licha ya kuwa nilikuwa nimeacha kunywa vileo",alisema.

Wema amesimulia kutofurahishwa na maneno machungu aliyoyasema mamake mbele ya umati mbele ya marafiki zake  akisema jambo hilo alingefaa kutangazwa mahali kama hapo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved