Mwigizaji na sosholaiti Vera Sidika ameonyesha kutoridhika baada ya aliye kuwa mumewe Brown Mauzo kuchapisha picha za mwanao kwenye kurasa za kijamii zinazoweka uso wake wazi.
Vera ambaye alirejea nchini hivi juzi baada ya kukamilisha muda wa likizo yake Marekani,ameshiriki katika ukurasa wake wa Insta,akiuliza sababu za kuchapisha picha za mtoto wao bila ya hata kujulishwa.
Ila pia alishiriki picha akiwa amembeba mwanaye mkononi ambayo pia iliweka uso wazi na kusema pia hana budi.
"Ilibidi tu,ila mbona kuchapisha bila hata kunijulisha?"
Alichapisha ujumbe huo huku akiwa amembeba mwanaye mkononi,akimtakia afya njema na baraka za Mungu na kusema atafanya kila juhudi kuhakikisha maisha ya mwanaye yamekuwa bora.
Brown Mauzo alimtambulisha mwanaye kwa mara ya kwanza kwa mashabiki.
Alishiriki picha ya mtoto wake Ice Brown katika ukurasa wa Insta kwa mara ya kwanza huku akichapisha ujumbe wa kumsifia mwanaye.
"Simba, prince Ice Brown," aliandika
Chapisho la mauzo linakuja siku chache baada ya Vera kutamka maneno ya kumdhalilisha baada ya kurudi nchini kutoka ziara zake marekani
Vera alisema kuwa hawana uhusiano na Mauzo na kumtaka kuwa mbali na yeye akisema hataki kumuona karibu yake.
“Sitaki kumuona Brown Mauzo popote karibu yangu. Nijuavyo, tumeachana, lakini itachukua muda kabla ya talaka kuisha," alisema.
Pia alikanusha madai kwamba Mauzo alionekana na gari lake siku chache baada ya kutangaza kuwa walikuwa wametengana.
"Gari langu lililo na nambari yangu, mtu pekee anayeendesha gari langu ni kaka yangu," Vera alifafanua.
Hata hivyo,hakuna hata mmoja kati ya hawa wawili aliyeshiriki picha zinazoweka wazi uso wa mwanao katika kurasa za mitandao ya jamii