logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Unaita bwana ya wenyewe 'Muevelasting'-Nyamu ajibizana na shabiki mtandaoni

Karen Nyamu na maoni ya kejeli alikanusha kuwa hakuwa akimrejelea Samidoh na kwamba alikosea.

image
na

Habari24 October 2023 - 04:41

Muhtasari


โ€ขKatika chapisho hilo Karen Nyamu alimtaja Samidoh kama "mwenye hasira kali" jambo ambalo lilimkasirisha shabiki aliyejibu madai kuwa yeye ni mnyakuzi wa mume.

โ€ข"Nilifurahishwa sana na Arteta, leo tupige pole  pole,tusipigwe kama  Man City na Man U kwa sababu muevelarsting ni timu ya chelseaโ€ 

Seneta Karen Nyamu/Instagram

Seneta wa kuteuliwa, Karen Nyamu alichapisha kwenye  ukurasa wake wa Facebook kuipongeza  Chelsea kwa kutoka sare na Arsenal.

Mwanasiasa huyo  alifarijika kwamba timu hiyo ya Chelsea hawakuicharaza Arsenal kwa vile Samidoh ni shabiki wa Chelsea.

Katika chapisho hilo Karen Nyamu alimtaja Samidoh kama "mwenye hasira kali" jambo ambalo lilimkasirisha shabiki aliyejibu madai kuwa yeye ni mnyakuzi wa mume.

"Nilifurahishwa sana na Arteta, leo tupige pole  pole,tusipigwe kama  Man City na Man U kwa sababu muevelarsting ni timu ya chelsea” Karen Nyamu aliandika.

Shabiki mmoja kwa jina,Murugi Mwinjah,pindi tu alipoona chapisho hilo alimshambulia Nyamu,kakisema atawezaje kumuita bwana ya mtu ivo.

“Ni bwana ya wenyewe unaita mueverlasting??? Team blue” Murungi Mwinjah alichapisha maoni yake kujibu Nyamu.

Katika kujibu kwa haraka, Karen Nyamu na maoni ya kejeli alikanusha kuwa hakuwa akimrejelea Samidoh na kwamba alikosea.

Wakosoaji wengine walidai kuwa mwimbaji huyo wa Mugithi hatimaye angemwacha na kurudi kwa Edday Nderitu na watoto wake.

"Ilikuwa siku ambayo Edday alikutana na Karis mtoto wa daktari kutoka kitui,,,๐Ÿ˜๐Ÿ˜ kitakuramba๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜" shabiki aliandika.

“Usiseme meverlasting......sema Nimsnatching...... nafikiri utaona hii๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™Š๐Ÿ™Š๐Ÿ™Š” Shabiki mwingine aliandika.

Mashabiki hao waliendelea na kumtania Nyamu huku wakimrushia maneno cheche za maneno amabyo yanapinga uhusiano wake na Samidoh

"Muevelasting my foot...hizo ni ndoto za mchana...lakini hata kama wewe ni mwakilishi ni Mungu atakuhukumu tu.." Shabiki alimkosoa.

Karen Nyamu kwa muda sasa amekuwa akiibua mijadala mitandaoni tangu kujihusisha kwake na Samidoh.

Hata hivyo,Nyamu alikwenda mbele kutangaza kwamba hatashiriki mume wake na mtu mwingine yeyote na alikuwa akipata nguvu kutoka kwa imani yake ya moyo ili kukabiliana na misukosuko yote.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved