Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Pwani, waliandaa hafla ya kuomboleza kifo cha mwanafunzi mwenzao Faith Adongo aliyeuawa Oktoba 20 kwa kuasha mishumaa kwa heshima yake.
Hafla hiyo ilipangwa na kikundi cha undugu wa wanafunzi huku yake yakitarajiwa kufanyika baadaye nyumbani kwao Homa Bay.
Diana Wanjiru,ambaye ni kiongozi wa wanafunzi,aliwalika wanafunzi wenzake kwa minajili ya kuchangisha kusaidia katika gharama ya mazishi.
"Kwa hivyo,nitowe wito kwa wanafunzi wote kwa ajili ya hafla kubwa ya kuchangisha fedha na kuwasha mishumaa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwenzetu. Sote tujitokeze kwa shehima ya mwenzetu,"alisema.
Picha za hafla hiyo zilionyesha wanafunzi hao wakiungana na kuwasha mishumaa huku wakifanya maombi na kuimba nyimbo za kufariji.
Hata hivyo, wanafunzi hao walitoa wito kuwepo kwa haki kwa mwenzao,na kuomba serikali kuimarisha usalama katika maeneo hayo.
Faith Adongo,aliripotiwa kufariki baada ya kuvamiwa na kudungwa kisu usiku wa Oktaba 20,alipokuwa akirejea nyumbani.
Alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ya kilifi,ila kwa bahati mbaya akaaga dunia kwa kuvuja damu nyingi.
Vifo vya wanafunzi hasa wa vyuo vimeshuhudiwa mfululizo kwa katika muda wa hivi punde.
Katika tukio tofauti,mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Daystar,naye aliaga dunia kwa njia tatanishi,ambapo uchunguzi unaendelea kubaini kifo hicho.
Kifo cha Mercy Cherono,pia kilijiri siku chache baada ya kusajiliwa katika chuo hicho,ambapo walikuwa wamehudhuria tamasha la wanafunzi wapya.