logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pata watoto na wanaume wako na akili - Matubia awashauri kina dada

Mapema mwaka huu Matubia, alitangaza kuwa wametengana na aliyekuwa mpenzi wake Blessing Lung'ahu

image
na

Habari02 November 2023 - 08:56

Muhtasari


• Akizungumza kwenye video iliyoshirikishwa kwenye ukurasa wa Insta, Matubia aliwashauri wanawake kupata watoto na wanaume ambao wako tayari kuchukua majukumu ya kuwalea wanao.

• "Mkiamua kupata watoto,pateni watoto na watu wako na akili,"

Jackie Matubia

Mwigizaji na muunda maudhui,Jacky Matubia,amejitokeza wazi kuwashauri wanawake ambao wako kwenye ndoa kuhusu swala la kupata watoto.

Akizungumza kwenye video iliyoshirikishwa kwenye ukurasa wa Insta, Matubia aliwashauri wanawake kupata watoto na wanaume ambao wako tayari kuchukua majukumu ya kuwalea wanao.

"Mkiamua kupata watoto,pateni watoto na watu wako na akili,"alisema.

Matubia,hata hivyo alisema kuwa si kwamba yeye yuko mkamilifu kwa maswala ya ndoa, ila alionelea ni vyema kuwatahadharisha wale ambao wako kwenye mahusiano na wana azma ya kupata watoto.

"Hata mimi kiliniramba, lakini uzuri wangu napenda kuwa mkweli,na kuzungumza ukweli jinsi ulivyo, maana ndilo jambo ambalo hunipa furaha."

Hata hivyo, maneno ya Matubia yanaonekana kumlenga baba ya mtoto wake ambaye walitengana hivi karibuni.

Mapema mwaka huu, Jacky Matubia,alichapisha kwenye ukurasa wake wa Insta akitangaza kuwa wametengana na aliyekuwa mpenzi wake Blessing Lung'ahu baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka miwili.

Matubia hajaonekana wazi au kutangaza kukumbwa na mawazo,bali amekuwa kila mara akionekana mchangamfu na mcheshi kuashiria jinsi alivyopokea uamuzi uo.

Hivi sasa,kuna mijadala ya hisia mbali mbali zinazomhusisha Matubia na Milly Chebby kuhusiana na hali ya urafiki wao.

Milly na Matubia walikuwa marafiki wa kufa kupona ambao walitangamana kwa undani zaidi kama ndugu wa toka nitoke, hali ambayo kwa sasa haishuhudiwi kamwe.

Hali hii ya kuzorota kwa urafiki wao,hata hivyo iliibuka pale Matubia alipokosa kuhudhuria sherehe za ndoa ya kitamaduni ya Milly Chebby, jambo ambalo limesababisha wawili hawa kukashifiana mitandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved