logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kiongozi wa Liberia George Weah apongezwa baada ya kukubali kushindwa

Kwake Weah, haikuwa tu hatua ya mwanamichezo mkubwa bali "alama ya juu ya uongozi na amani".

image
na Radio Jambo

Habari21 November 2023 - 04:29

Muhtasari


•Rais wa Liberia George Weah amesifiwa kwa hatua yake ya kuonyesha 'uanaspoti mzuri' kwa kukubali kushindwa.

•Simu ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 ya kumpongeza Joseph Boakai siku ya Ijumaa usiku imeiokoa nchi hiyo.

George Weah

Rais wa Liberia George Weah amesifiwa kwa hatua yake ya kuonyesha 'uanaspoti mzuri' kwa kukubali kushindwa na mpinzani wake katika kinyang'anyiro cha urais na viongozi wa kutoka pande za kisiasa ana kanda ya Afrika Magharibi .

"Huu ni wakati wa neema katika kushindwa, wakati wa kuweka nchi yetu juu ya chama, na uzalendo juu ya masilahi ya kibinafsi," nyota huyo wa zamani wa kandanda, ambaye amehudumu kama rais wa Liberia tangu 2018, alisema.

Simu ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 ya kumpongeza Joseph Boakai siku ya Ijumaa usiku imeiokoa nchi hiyo, ambayo ina historia ya migogoro ya kikatili ya wenyewe kwa wenyewe, kutoka wikendi ya mvutano.

"Hizi ni nyakati nzuri nchini Liberia na barani Afrika kwa sababu hatua kama hiyo kwa upande wa rais aliyeko madarakani ni nadra sana," mtetezi wa haki za binadamu wa Liberia Hassan Bility aliiambia BBC.

Yeye ni mkurugenzi wa Mradi wa Haki na Utafiti wa Kimataifa (GJRP), ambao umekuwa ukiandika ushahidi wa uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo takriban 250,000 walikufa.

Kwake yeye, kwa Bw Weah kukubali kushindwa katika duru ya pili - siku tatu kabla ya matokeo rasmi kutangazwa - haikuwa tu hatua ya mwanamichezo mkubwa bali "alama ya juu ya uongozi na amani".

Rais ana 49.11% ya kura hadi sasa kutoka kwa matokeo ya 99.58% ya vituo vya kupigia kura.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved