logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkanganyiko mchezaji akipiga mpira header kutoka mikononi mwa kipa na bao kukubaliwa (video)

Lakini tukio la bao hilo kukubaliwa limesaliwa kuwa lenye maswali na ukosoaji mwingi.

image
na Radio Jambo

Habari23 November 2023 - 06:18

Muhtasari


• Sare hiyo ilionekana kumalizika kwa sare ya 2-2 kabla ya Besiktas kufunga bao la ushindi katika dakika ya 95 ya sare hiyo.

Bao la ajabu

Kulishuhudiwa na mkanganyiko mkubwa katika mecho ya soka ya wanawake nchini Uturuki wakati mchazaji wa timu pinzani alipomvizia kipa na kupiga header mpira kutoka mikononi mwa kipa kabla ya kupiga shuti langoni.

Cha ajabu Zaidi ni kwamba refa alihalalisha bao hilo na kuzua utata Zaidi kutoka kwa wachezaji uwanjani lakini pia wachambuzi wa soka kote ulimwenguni.

Mechi hiyo ya wanawake ilikuwa kali na ya debi baina ya mahasimu wa muda mrefu, Fenerbahce and Besiktas.

Sare hiyo ilionekana kumalizika kwa sare ya 2-2 kabla ya Besiktas kufunga bao la ushindi katika dakika ya 95 ya sare hiyo.

Kivangaito kilishuhudiwa wakati Besiktas walikimbia na mpira langoni mwa mpinzani lakini mlinda lango akasimama tisti kabisa na kushika mpira ule.

Wakati golikipa aliwa anawapanga wachezaji wenzake kusonga mbele ili awatupie mpira katikati ya uwanja, mchezaji wa timu pinzani alimkaribia na kupiga kichwa mpira kutoka mikononi mwake.

Mpira huo ulidondoka uwanjani na mchezaji huyo akausindikiza langoni kwa shuti hafifu kabla ya kuanza kusherehekea.

Wachezaji wenzake mwanzoni walibung’aa na hawakuharakisha kujiunga naye kusherehekea kabla ya refa kupuliza kipenga akionesha ishara ya mpira kupelekwa katikati ishara kwamba bao limesimama.

Hata hivyo, wachezaji wa Besiktas walimvania refa kwa maswali mengi jambo lililomghilibu na akatoa kadi za njano.

Lakini tukio la bao hilo kukubaliwa limesaliwa kuwa lenye maswali na ukosoaji mwingi kwani golikipa tayari alikuwa ameushika mpira mikononi mwake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved