Makamu wa rais wa Chama cha Wanasheria nchini, Faith Odhiambo amelitaka baraza la mitihani KNEC kukagua matokeo ya KCPE ambayo yalitolewa ili kushughulikia maswala yaliyoibuliwa
Baraza hilo la Kitaifa la Mitihani la Kenya limekuwa likikabiliwa na mzozo tangu kutolewa kwa matokeo ya KCPE Alhamisi iliyopita baada ya malalamishi mengi kuibuka miongoni mwa watainiwa.
Kutolewa kwa matokeo hayo pia kulikumbwa na kucheleweshwa kwa jukwaa fupi la msimbo wa SMS, hitilafu ambayo shirika hilo limesema lilikuwa likichunguza.
Baadhi ya masuala yaliyoibuliwa yalikuwa ya alama zinazofanana kwa somo moja katika darasa zima.
Baraza hilo la Knec tangu wakati huo imefafanua kuwa mfano wa alama zinazofanana kwa darasa zima haukuwa kama udanganyifu au ukiukaji wa utaratibu.
Naibu wa rais wa LSK alisema kuwa baraza la mitihani linafaa kuharakisha kushughulikia maswala hayo kwani wanafunzi wengi hawana amani hata msimu wa sherehe unapokaribia.
Hata hivo alindokeza kuwa baraza hio imeaminika kwa miaka mingi na inafaa kudumisha heshima hiyo kwa kukagua motokeo hayo tena.
“Baraza la mitihani kwa muda mrefu limepata heshima ndani na nje ya nchi kwa rekodi ndefu ya mitihani ya kuaminika,"alisema.
Baadhi ya Wabunge wameibua wasiwasi kuhusu dosari za matokeo ya KCPE. Wakiongozwa na Mbunge wa Tinderet Julius Melly na mbunge wa Marakwet Magharibi Timothy Kipchumba Toroitich, wabunge hao wamefichua mipango ya kumwita Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu kuelezea utepetevu bungeni.