Msichana mrembo mwenye kisomo cha haja katika taaluma ya uuguzi amewashangaza wengi katika mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba licha ya urembo wote alio nao, hakuna mwanamume amewahi mfuata kutaka kuwa mpenzi wake kwa miaka minne sasa.
Mrembo huyo kwa kuhisi kwamba pengine huenda kuna jambo ambalo haliko sawa na yeye, aliamua kutafuta huduma ya maoni kwa mtumizi mmoja wa mitandaoni anayechapisha matatizo ya watu ili kupata maoni kutoka kwa watumizi wa mitandao ya kijamii.
Kwa kuanzia, mrembo huyo alibainisha kwamba yeye ana umri wa miaka 24 na ni mrembo kupindukia, akisisitiza kuhusu rangi nyeupe ya ngozi yake – rangi ambazo zinakisiwa kuwavutia wanaume wengi – lakini pia yeye ni mtu na taaluma yake maridadi, kinachomsumbua tu ni kutopata mapenzi.
“Hili limekuwa likinichanganya akili sana, na ningependa kusikia maoni ya watu kulihusu. Mimi ni mrembo mwenye umri wa miaka 24, mwenye ngozi nyeupe Zaidi na mrembo [ila siringi], mimi pia ni mhudumu wa afya, nisichokielewa ni kwamba wanaume wengi hawataki kunitongoza,” alisema.
Mrembo huyo aizidi kujieleza na kusema kwamba amekuwa bila mpenzi tangu mwaka 2019 licha ya kubarikiwa na urembo wa kumfanya kila mwanamume kugeuza shingo mara mbili mbili pindi wanapopitana njiani.
“Nimekuwa bila mpenzi tangu 2019, nimekuwa mpweke kwa muda mrefu na pia nimekuwa katika mahusiano ya kubahatisha yasiyo na mwelekeo tangia hapo. Nimegundua kwamba hakuna mwanamume anayetaka kutumia hata senti kwangu, huwa sioneshi dalili za kukaa msichana wa kitajiri lakini pia hata hivyo sijawahi bahatika,” alijieleza.
Pia alihisi kwamba pengine tatizo liko upande wake kwani kila mara anapopatana na mwanamume, hajawahi msikia mwanamume akifunguka kujitolea kumpeleka katika mtoko wa kujivinjari na kufurahia muunganiko wao.
