Wapenzi wa nyimbo za kutoka ukanda wa Magharibi wa Kenya wametupwa kweney kipindi cha maombolezo kufuatia kifo cha msanii wa bendi ya Phonotex ambayo inaongozwa na msanii maarufu Jacob Luseno.
Gertrude Mwendo Anyika, ambaye alifahamika na wengi kwa sauti yake ya kuvutia katika kibao maarufu kwa jina ‘Mukangala’ alitangazwa kufariki usiku wa kuamkia Desemba 17 baada ya muda mrefu wa kupambana na saratani, taarifa zilisema.
Anyika alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Moi jijini Eldoret.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanablogu Mwalimu Amunga Akhanyalabandu alithibitisha kifo cha Anyika mnamo Ijumaa, Desemba 15.
"Gertrude amekuwa hospitalini kwa miezi kadhaa akiugua saratani. Bili zake kubwa zilikuwa KSh 2.5 milioni, ambazo familia haikuweza kulipa. Alikuwa katika wadi ya umma. Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi huko Eldoret," Amunga alichapisha kwenye X.
Anyika ni sauti maarufu ya kike katika Bendi ya Phonotex Success, iliyoanzishwa na marehemu Jacob Luseno mnamo 1965.
Alirekodi nyimbo nyingi zilizovuma akiwa na Luseno. Wimbo maarufu zaidi ni Mukangala na Amakuru, uliorekodiwa mwaka wa 1974.
Nyimbo nyingine ni pamoja na Injeti, Masiali, Cecilia, Regina, House Maid, Bushuma Bwa Malika, Ingato, na Linda, miongoni mwa nyimbo zingine