logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ujumbe mtamu wa Barack Obama kusherehekea mkewe kwa kufikisha miaka 60

"Siwezi kusubiri kuona nini muongo huu mpya utakuletea,”       Obama aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari18 January 2024 - 10:53

Muhtasari


• “Hivi ndivyo 60 inavyoonekana. Furaha ya kuzaliwa kwa nusu yangu bora - ambaye anatokea kuwa mmoja wa watu wa kuchekesha, werevu zaidi, mrembo zaidi ninayemjua."

MICHELLE OBAMA, MKEWE BARACK OBAMA

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama amemsherehekea mkewe, mama Michelle Obama kwa kufikisha umri wa miaka 60.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Obama alichapisha picha ya mkewe na kufichua kwamba amefikisha umri wa miaka 60, huku akimtaja kuwa mmoja wa watu waungwana sana wa karibu naye.

Rais huyo wa awamu ya 44 wa Marekani alimtakia kila la heri mkewe, akisema kuwa ni mcheshi ambaye hatosubiri kuona muongo huu mwingine wa miaka ya 60s utakuwa vipi wakiwa pamoja.

“Hivi ndivyo 60 inavyoonekana. Furaha ya kuzaliwa kwa nusu yangu bora - ambaye anatokea kuwa mmoja wa watu wa kuchekesha, werevu zaidi, mrembo zaidi ninayemjua. Michelle Obama, unafanya kila siku kuwa bora. Siwezi kusubiri kuona nini muongo huu mpya utakuletea,”       Obama aliandika.

Mashabiki wa familia hiyo walionesha mshangao wao kujua kwamba Michelle amefikisha umri wa miaka 60 licha ya kuwa na ngozi laini na mbichi.

“Siku ya kuzaliwa yenye furaha na kwa kweli, huonekani mwenye umri wa Zaidi ya miaka 28. Namaste, nakutakia kila la heri.” Heidi De La Teja alisema.

“Siku ya kuzaliwa yenye furaha na ndiyo 60 inaonekana nzuri kwako. Karibu kwa wafanyakazi 60 plus.♥️” Sahron Paige.

“Heri ya kuzaliwa kwa utu wa uzuri na nguvu. Asante na Barack kwa ubora na utu wako,” mwingine alisema.

Baadhi ya watu wanamshinikiza Michelle kujitosa katika siasa na kuwania urais pindi rais wa sasa Joe Biden atakapomaliza mihula yake miwili – kama atachaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa mwishoni mwa mwaka.

Wengi wamekuwa wakimsifia Michelle kama mama wa taifa ambaye alikuwa mzuri kipindi cha uongozi wa Obama kama rais kati ya 2008 hadi 2016.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved