Siku ya valentines ni siku ambayo wapenzi duniani kote wanasherehekea mapenzi. Wengi wa wapendanao hununuliana zawadi mbali mbali.
Sanasana wao hununuliana maua na chokoleti. Leo tutaangalia maua tofauti tofauti ambayo unaeza nunulia mpenzi wako na maana zao.
Ua la Tulips
Maua hizi zinajulikana sana kwanza siku ya valentines.
Tulips waridi inaashiria upendo na urafiki.
Tulips zambarau inaashiria mrabaha.
Tulips njano inaashiria furaha.
Tulips nyeupe inaashiria msamaha pamoja na usafi na ya mwisho ni tulips nyekundu ambayo inaashiria upendo.
Ua la waridi
Hii maua ndio inayojulikana sana na wapenzi wakifikiria valentines. Wengi wanajua tu ua la waridi nyekundu lakini kuna tofauti tofauti ambazo ziko na maana zao.
Tuko na nyeupe ambayo inaashiria usafi na upendo wa milele.
Njano inaashiria urafiki.
Waridi inaashiria umaridadi.
Mrujuani inaashiria siku ya kwanza mulipo kutana na la mwisho ni nyekundu ambayo inaashiria upendo na hiyo ndio wengi wao hujua.
Ua la Karafu
Ua hili inawakilisha kujitolea na mapenzi. Ua hili pia iko na rangi tofauti tofauti ambazo ziko na maana zao.
Waridi inaashiria shukrani.
Nyeupe inaashiria usafi na urafiki.
Nyekundu kama kawaida inaashiria upendo. Kuna pia ya rangi njano lakini epuka kumtumia mpenziwe hiyo kwa sababu inaashiria kukataliwa.
Ua la Peonies
Ua hili inawakilisha furaha, kukuwa aibu, mapenzi,bahati nzuri, heshima na ushujaa. Hii pia iko na rangi lakini ni moja tu ambayo ni waridi na inaashiria ustawi,bahati nzuri na furaha.
Ua la Alizeti
Ua hili pia inajulikana sana kwa sababu ya urembo wao na rangi pia. Huwa inwakilisha pongezi na kujitolea kwa mpenzi wako na urafiki.