logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu waliokamatwa kwa kwenda nyumbani kwa Kiptum waachiliwa huru

Wanaume hao wanne pia wanajulikana na wanafamilia wa Kiptum na mpaka wamekutano nayo.

image
na Radio Jambo

Habari15 February 2024 - 05:13

Muhtasari


  • Kampuni hiyo ilifaa kusambaza nguo za spoti ambazo Kiptum alifaa kutumia  katika Chicago marathon.
  • Washukiwa hao walieleza polisi kuwa kampuni ilituma wanaume hao wanne ili mwanariadha huyo aweze kutimiza wajibu wa mkataba wake. 

amefariki akiwa na umri wa miaka 24.

Washukiwa wanne ambao walizuru nyumbani kwa bingwa wa marathon Kevin Kiptum siku kadhaa kabla ya kifo chake wameeleza nia yao.

Washukiwa hao walieleza kuwa walienda nyumbani kwake kujadiliana na Kiptum kuhusu mkataba wa milioni 45 ambao alikuwa amesaini na kampuni ya Wachina ambayo mwanariadha huyo alichagua kughairi mpango huo na kulipa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ilifaa kusambaza nguo za spoti mabazo Kiptum alifaa kutumia siku ya marathon ya Chicago na inadaiwa kuwa mwanariadha huyo alikuwa anaenda kutumia nembo nyingine na si hiyo ya Wachina.

Afisa wa uchunguzi wa uhalifu Elegeyo Marakwet, Joshua Chelele alieleza kuwa kwa hayo yote washukiwa wameeleza, ni ukweli kuwa hawakuwa na nia ya kumuua mwanariadha huyo.

Washukiwa hao walieleza polisi kuwa kampuni hiyo ilituma wanaume hao wanne ili mwanariadha huyo aweze kutimiza wajibu wa mkataba. 

Kelvin Kiptum

"Wameeleza nini na sababu yao ya kwenda nyumbani mwa Kiptum. Uchunguzi bado unaendelea na watarudi Ijumaa kama inatakikana".

Alieleza kuwa wanaume hao wanne pia wanajulikana na wanafamilia wa Kiptum na mpaka wamekutano nayo.

Haya mambo yote yaliibuka wakati babake Kiptum alisema kuwa kuna wanaume wanne walimtembelea nyumbani kwake siku nne kabla ya kifo ya mtoto wake na kumuuliza kuhusu Kiptum na hiyo iliibua kengele.

Mazishi ya Kiptum imepangwa kukuwa Februari 24.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved