logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati na Diana Marua washangaza mashabiki kwa kutumia mswaki mmoja kwa zamu (video)

โ€œUongo mbaya! Siwezi kushiriki mswaki wangu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ afadhali mninyonge,โ€ Njambi Fever.

image
na Radio Jambo

Habari27 February 2024 - 07:45

Muhtasari


โ€ข Bahati walisema ni ishara ya mapenzi wengine wakipinga kwa kauli kwamba huo ni ukichaa katika mapenzi.

 

Bahati na mkewe Diana

Wakuza maudhui Diana Marua na Kevin Bahati wamewaacha mashabiki na watumizi wa mtandao wa Instagram katika hali ya mshangao baada ya kupakia video wakishiriki kupiga mswaki kwa kutumia mswaki mmoja.

Wawili hao walionekana katika hali ya furaha huku kila mmoja akiuchukua mswaki huo huo mmoja kwa zamu kutoka kwa mdomo wa mwenzake.

Baadae hata kabla ya kusukutua, Diana alionekana akitaka kumbusu Bahati kabla ya wote kucheka.

Waliandika;

“Yako ni Yangu; Yangu ni Yako โค๏ธ Nitang’a Ng’ana Nawe ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.”

Hatua hii ya kubadilishana mswaki kutoka kwa mdomo wa Bahati kwenda kwa mdomo wa Diana na kurudia ilivutia maoni tofauti kutoka kwa mashabiki wao.

Bahati walisema ni ishara ya mapenzi wengine wakipinga kwa kauli kwamba huo ni ukichaa katika mapenzi.

โ€œUongo mbaya! Siwezi kushiriki mswaki wangu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ afadhali mninyonge,โ€ Njambi Fever.

โ€œDiana siuko na bahati ,unaishi kimalaika utaenda Heaven direct,โ€ Eddy Musomb alisema.

โ€œNikifika hapa mnipige risasi ya figo.โ€ Sebastian Obk.

โ€œUwiiiii nimehisi kutapikaaโ€ Zahras Choice alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved