logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari Hassan amfanyia mumewe dua maalum; amuombea binti 2, kuto'cheat, jumba kubwa, afya...

Miongoni mwa vitu  ambavyo alijiombea ni baraka nyingi kwa watoto wake, mali zaidi, maisha mazuri na amani.

image
na Radio Jambo

Football08 April 2024 - 12:05

Muhtasari


•Zari alisikika akitaja vitu ambavyo wangetaka kujaliwa navyo huku mumewe akisema ‘Amina’ baada ya kila kitu kilichotajwa.

•Miongoni mwa vitu  ambavyo aliomba ni baraka nyingi kwa watoto wake, mali zaidi, maisha mazuri na amani.

Mwanasholaiti maarufu wa Uganda Zari Hassan na mumewe Shakib Cham Lutaaya hivi majuzi walifanya maombi ya pamoja ambapo walimwomba Mungu awape vitu kadhaa maalum.

Katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Zari alisikika akitaja vitu ambavyo wangetaka kujaliwa navyo huku mumewe akisema ‘Amina’ baada ya kila kitu kilichotajwa.

Mama huyo wa watoto watano alianza kwa kutaja vitu ambavyyo angetaka Shakib apewe ikiwa ni pamoja na gari la kifahari, jumba kubwa la kifahari, mabinti wawili na uaminifu katika ndoa.

“Namuombea G-Wagon kubwa Nyeusi mume wangu, naomba biashara kubwa kwa mume wangu, namuombea watoto wawili wa kike mume wangu, namuombea nyumba kubwa mume wangu,” Zari alisema huku Shakib akikubali kwa kusema ‘Amina. '.

Mwanasosholaiti huyo aliongeza, "Ninaombea safari, safari, safari na safari zaidi mume wangu. Ninaombea shughuli nyingi za ununuzi na likizo Dubai, naomba kusafiri kwa ndege za kibinafsi, ninaombea maisha marefu, afya, amani, upendo wa milele, hakuna udanganyifu, hakuna kurukaruka, hakuna kutongozana nje..”

Baada ya kuomba vitu kadhaa maalum mumewe, mzazi mwenza huyo wa staa wa bongofleva Diamond Platnumz naye  pia aliomba vitu kadhaa kwa ajili yake.

Miongoni mwa vitu  ambavyo aliomba ni baraka nyingi kwa watoto wake, mali zaidi, maisha mazuri na amani.

"Najiombea G-Wagon kubwa la pinki, naomba maisha marefu kwa watoto wangu, naombea watoto wetu pesa nyingi, naomba almasi nyingi na Rolex na kila kitu.

Naomba amani, naomba uridhi mkubwa wa familia yangu, naomba kuweka kila kitu, kuwa na afya, naomba janam, maisha mazuri, naomba imani na amani. Inshaalah imekamilika,” Mwanasosholaiti huyo aliomba.

Video hiyo pia ilionyesha upendo mkubwa kati ya wanandoa hao kutoka Uganda kwani walionekana kufurahia kufanya maombi hayo maalum pamoja.

Zari na Shakib walirasimisha ndoa yao katika harusi ya faragha iliyofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwezi uliopita. Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maelezo ya harusi hiyo yalikuwa yamefichwa sana lakini tulifanikiwa kupata baadhi ya picha na video za sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu kwa mara ya kwanza katika harusi ya kidini ya Kiislamu (Nikah) mapema mwaka huu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved