logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Tap! Tap!” MP Salasya ajiunga TikTok, aomba watu kumtumia zawadi

Huyu si mwanasiasa wa kwanza kujiunga katika mtandao huo wa video fupi.

image
na Radio Jambo

Habari27 April 2024 - 11:02

Muhtasari


• Mnamo Ijumaa tarehe 26 Aprili 2024, Peter Salasya aliendelea na TikTok Live ili kutangamana na mashabiki wake kwa kuomba zawadi kutoka kwao.

PETER SALASYA

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amejiunga na TikTok Live na kuanza kuomba mashabiki wake zawadi kwa mtindo ambao umezoeleka wa ‘tap tap’.

 Baada ya kuingia, Salasya alifurahi na kusema kwamba alikuwa anataka kuwaona mashabiki wake kisha kuwaambia wamtumie zawadi mbali mbali.

Mnamo Ijumaa tarehe 26 Aprili 2024, Peter Salasya aliendelea na TikTok Live ili kutangamana na mashabiki wake kwa kuomba zawadi kutoka kwao.

“Mnitumie maua, nitumie kofia, nitumie ile nembo ya tiktok, zote tuma sasa hivi, nataka kuwaona watu wangu, napenda TikTok yangu, sema tap tap screen tap tap mnasema tap tap, acha nisome zaidi,” Salasya alisema huku mashabiki wake wakimmiminia zawadi ainati.

Mashabiki hawakumkasirisha bali walimtumia emojis za waridi na kofia kwenye sehemu ya maoni ili kumsumbua.

Huyu si mwanasiasa wa kwanza kujiunga katika mtandao huo wa video fupi.

Itakumbukwa miaka miwili iliyopita, gavana wa Nyeri alikiri kuwa mmoja wa watu wanaopenda mtandao huo, akisema kuwa anautumia kama njia moja ya kufikia vijana na kupata maoni yao kuhusu uongozi wa Nyeri.

Viongozi wengine ambao wanatumia TikTok ni pamoja na gavana wa Nairobi Johnson Sakaja na seneta mteule Karen Nyamu.

Hata hivyo, Salasya anakuja kama mwanasiasa wa kwanza kujiunga na kwaya ya kuwarai mashabiki kufanya tap tap na kumtumia zawadi.

Hivi majuzi, mchungaji mwenye utata Victor Kanyari alijiunga katika mtandao huo na mara kwa mara amefanya kama mtindo kuenda live akiomba mashabiki kumtumia zawadi.

Hata hivyo, Kanayri aliweka wazi kwamba hakufuata zawadi za pesa kwenye tiktok bali alifuata vijana waliokaliwa na ibilisi ili kuwahubiria.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved