logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Daktari alidhani sifanyi mapenzi kwa sababu ya ulemavu

Watkins ana ugonjwa wa mifupa, ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika kwa wepesi.

image
na Radio Jambo

Habari17 May 2024 - 04:56

Muhtasari


• Kat Witkins alihisi kutendewa vibaya kama sio binaadamu, licha ya kuwaambia wafanyakazi wa matibabu namna bora ya kuuweka mwili wake.

Kat Watkins anadai kuwa amepitia mambo ya kutisha katika kliniki na hospitali.

Kat Watkins, mwanamke anayetumia kiti cha magurudumu, anasema daktari alidhani hakuwa akifanya ngono kwa sababu ya ulemavu wake.

Watkings, mwenye umri wa miaka 37 na mkazi wa Swansea, nchini Uingereza, pia anasema alipokuwa akifanyiwa kipimo cha uzazi walimwambia alikuwa na "mwili wa ajabu sana."

Yeye ni mmoja kati ya watu wazima 30 ambao waliiambia BBC huko Wales kwamba walikumbana na changamoto katika kupata huduma za afya kwa sababu ya ulemavu wao.

Serikali ya Wales ilisema imesikitishwa sana kusikia visa hivi.

Maelezo ya picha,Kwa sababu ya hali yake, Kat anapata majeraha ya mara kwa mara

Kwa sababu ya hali yake, ya ugonjwa wa mifupa, ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu na kuvunjika kwa wepesi, Watkins anasema kupata matibabu sahihi ni tabu sana.

Anasema huepuka kwenda kwenye matibabu kwa sababu ya mambo aliyokutana nayo zamani.

"Nimekuwa nikipigana kwa miaka 37 ili kushinda vikwazo na bado vipo. Kwangu mimi ni zaidi ya vikwazo, ni vita vya mara kwa mara," anasema.

Watkins anaeleza mtu ambaye alimfanyia uchunguzi wa magonjwa ya uzazi alisema asipange tena miadi katika siku zijazo kwa sababu hakuwa akifanya ngono.

"Alikuwa akidhani kuwa sikufanya ngono kwa sababu mimi ni mlemavu," anaeleza.

Hiyo ilimaanisha Watkins alipaswa kurudi katika kiliniki mara kadhaa ili kupata matokeo.

Pia anasema alihisi kutendewa vibaya kama sio binaadamu, licha ya kuwaambia wafanyakazi wa matibabu namna bora ya kuuweka mwili wake.

Katika ziara nyingine katika hospitali hiyo, anasema alihisi wafanyakazi hawakumsikiliza wala kumwamini alipowaambia alikuwa amevunjika mifupa kadhaa kwenye mguu wake.

Baadaye ilithibitishwa kuwa mguu wake ulivunjika katika sehemu tano.

Bodi ya afya ya Swansea Bay ilisema haiwezi kutoa maoni juu ya kesi za mtu binafsi lakini ingefurahi kujadili jambo hilo na Watkins.

“Walishindwa kabisa”

Michelle Penny anasema hajawahi kufanya vipimo vya afya, kwa sababu ya kukosa fursa na kama ilivyo kwa Watkins, anaamini mfumo wa afya haujamtendea sawa.

Ugonjwa wa kuchoka kupita kiasi umemuweka kitandani na anapata ugumu kuondoka nyumbani kuhudhuria miadi yake ya matibabu.

"Kila mtu anahitaji aina fulani ya huduma ya afya, lakini kama huwezi kuipata, unakuwa umeshindwa," anasema.

Penny hajaonana na daktari kwa takribani miaka sita na ana miadi kuhusu pumu kupitia simu, lakini anasema hiyo haitoshi.

"Unaweza kuwaambia chochote na wataamini kwa sababu hawawezi kukuona," anaongeza.

Penny pia ameunga mkono wito wa vipimo vya nyumbani vya Human Papillomavirus, ambavyo kwa sasa vinajaribiwa nchini Uingereza.

Maelezo ya picha,Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu huadhimishwa tarehe 3 Desemba.

Alex Harrison, afisa wa masuala ya usawa kwa walemavu huko Wales, anasema watu wengi ambao wamekuwa na matatizo na huduma za afya hukata tamaa.

“Kutokana na hali hiyo hupata matatizo mapya au hali zao zimekuwa mbaya zaidi,” anasema.

"Wengi wanahisi wamepuuzwa tu au ziara za matibabu ni mzigo mkubwa sana kwao."

"Tunasikia mengi kwamba watu husubiri tu na kusubiri kupigiwa na hilo halitokei kamwe."

Anaamini ili kuleta mabadiliko, mafunzo ya usawa kwa walemavu, yanayofundishwa na mtu mlemavu na mawasiliano zaidi, yanahitajika.

Msemaji wa Serikali ya Wales alisema: "Inasikitisha sana kusikia hadithi hizi na tunatumai kuwa walemavu watasikilizwa na kutibiwa kwa heshima."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved