KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Mei 17.
Katika taarifa ya siku ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kisii na Murang'a.
Katika kaunti ya Kisii, baadhi ya sehemu za eneo la Ogembo zikiwemo Ogembo Sports Club, MRF Tyres, Junior Farms Ogembo, Getare Pri, Gituno TBC na viunga vyake zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Maporomoko na Ngoingwa katika kaunti ya Murang'a pia zitakosa huduma za umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
KPLC imesema kuwa mpango wa kukatizwa kwa umeme katika maeneo yaliyotajwa ni kutokana na matengenezo ya mtandao yatakayokuwa yakifanyika.