logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Roboti iliyoundwa nchini Tanzania yatambulishwa bungeni na kuwahutubia waheshimiwa (video)

Muda mfupi baadaye, picha na video za Roboti Eunice zimegeuka kuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

image
na Radio Jambo

Habari17 May 2024 - 05:49

Muhtasari


• Roboti Eunice ilikuwa ikiwakaribisha wageni waliokuwa wakiingia bungeni kusikiliza makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Roboti Eunice.

Alhamisi gumza pevu liligonga vichwa vya habari baada ya roboti ya kwanza kutengenezwa na wanateknolojia nchini Tanzania kutambulishwa katika majengo ya bunge.

Roboti hiyo iliyopewa jina Eunice ilifikishwa bungeni majira ya asubuhi na kuonekana ikifanya mazungumzo na baadhi ya wabunge kwa mshangao wa wengi.

Eunice ilikuwa ikiwakaribisha wageni waliokuwa wakiingia bungeni kusikiliza makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Muda mfupi baadaye, picha na video za Roboti Eunice zimegeuka kuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa wachangiaji, walionesha kufurahishwa na maendeleo ambayo Tanzania imepiga kwenye masuala ya teknolojia kiasi cha kumuunda Roboti Eunice mwenye uwezo wa kuongea na kupeana mikono na watu.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alikuwa miongoni mwa watu waliokaribiishwa na roboti Eunice wakati akiingia bungeni ambapo uwasilishaji wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024 / 2025, ulifanyika.

Katika baadhi ya video za kushangaza zilizonaswa kutoka kwa tukio hilo, Roboti hiyo iliyokuwa katika lango ya kuingia ukumbi wa Bunge lilitangamana na wabunge ambao pia walipata nafasi ya kuisamilia na kuiuliza maswali na roboti hiyo ikijibu.

Hizi hapa ni baadhi ya video wabunge wakitangamana na roboti Eunice katika majengo ya bunge;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved