logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Sitaki yeyote!" Mjukuu wa Kibaki, Sean Andrew afichua kwa nini hataki kupata watoto

Pia alidokeza kwamba ana mambo mengi zaidi ya kushughulika nayo.

image
na Radio Jambo

Burudani21 May 2024 - 05:36

Muhtasari


•Mjukuu huyo wa Hayati Emillio Mwai Kibaki aliweka wazi kwamba tayari ana shida za kutosha kuwashughulikia mbwa wake.

•Mwaka wa 2021, wakati aliulizwa iwapo amewahi fikiria siku moja kuoa na kutulia katika ndoa na kuwa na watoto.

Mwanamitindo na mtayarishaji maudhui maarufu wa Kenya Sean Andrew ameshikilia kuwa hana mpango wa kupata watoto sasa au katika siku zijazo.

Wakati akiwashirikisha wafuasi wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram siku ya Jumapili jioni, mjukuu huyo wa aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya, marehemu Emillio Mwai Kibaki alisema kuwa tayari ana shida za kutosha kuwashughulikia mbwa wake.

Pia alidokeza kwamba ana mambo mengi zaidi ya kushughulika nayo, jambo ambalo pengine limefanya kuwa mzazi kuwa hatua ambayo hataki kabisa kupiga.

“Utakuwa na watoto?” shabiki alimuuliza.

Sean alijibu, "Sitaki yeyote, nimepata shida zaidi za kutosha na (mbwa) hawa na zaidi."

Aliambatanisha jibu lake na picha ya mbwa wanne wakiwa wamelala kwenye sakafu.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 kuzungumza kuhusu suala la kutotaka kuwa na watoto.

Takriban miaka miwili iliyopita, aljibu swali la mtumizi mwingine wa mtandao wa Instagram aliyemuuliza  kuhusu suala kuwa na watoto na akasema amekuwa akijua tangu kitambo kwamba hataki kuwa baba.

“Mbona hutaki kuwa baba siku moja?” mmoja kati ya mashabiki wake aliuliza.

“Ni vile tu sitaki watoto. Hicho ni kitu nimekuwa nikijua kwa muda sasa,” alijibu Andrew.

Mwaka wa 2021, wakati aliulizwa iwapo amewahi fikiria siku moja kuoa na kutulia katika ndoa na kuwa na watoto.

Alijibu, “Ndio nimewahi fikiria kuoa na kutulia katika ndoa lakini hata siku moja sijawahi jifikiria au kujiona kuwa baba. Pengine niwe mume tu lakini sitaki watoto."

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved