KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Julai 11.
Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kajiado, Nyeri, Embu, Kiambu, na Kilifi.
Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Gigiri Whispers utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za eneo la Loitokitok katika kaunti ya Kajiado zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Ndunyo na Mahiga katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za eneo la Majengo katika kaunti ya Embu pia zithakosa umeme kati ua saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Katika kaunti ya Kiambu, mtaa wa Riara na hospitali ya Nazareth zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za eneo la Ganze katika kaunti ya Kilifi pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.