logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kisa kingine cha ugonjwa wa M-Pox chapatikana huku maambukizi yakifikia watu 14

Waziri wa Afya Dr. Deborah Barasa athibitisha kisa cha 14 cha gonjwa la Mpox - Uasin Gishu

image
na jacob kimanthi

Habari18 October 2024 - 10:04

Muhtasari


  • Wizara ya Afya kuendelea kufanya vipimo zaidi kwa viingilio vyo vya taifa kwa nchi za kigeni kufikia sasa vipimo takriban 1,362,657 zikiwa zimefanywa.
  • Kisa cha 14 chapatikiana kaunti ya Uasin Gishu na kufikisha visa vya maambukizi kuwa 14 na kifo kimoja .

Kisa cha 14 cha maambukizi ya Ugonjwa wa Mpox chapatikana kaunti ya Uasin Gishu.Wizara ya Afya imeweza kuthibitisha kisa hicho ambacho kinaongeza visa jumla kuwa 14 kufikia sasa humu nchini tangia kukurupuka kwa gonjwa hili.

Waziri wa Afya Dr. Deborah Barasa katika taarifa aliyoitoa mnamo tarehe  17 Oktoba alisema kisa hicho kilipatikana kaunti ya Uasin Gishu.

Visa hivi vya ugonjwa huu vimeweza kupatikana katika kaunti zifuatazo ndiposa kufikisha jumla ya visa 14:

  1. Nakuru - 2
  2. Bungoma - 2
  3. Taita Taveta - 1
  4. Busia - 1
  5. Nairobi - 1
  6. Mombasa - 1
  7. Makueni - 1
  8. Kericho - 1
  9. Kilifi - 1
  10. Uasin Gishu - 1

Waziri Barasa alidokeza kuwa kati ya visa hivyo,wagonjwa wanane wameweza kupona na watano wanaendelea kupokea matibabu ya kibinafsi hili kuregesha hali salama.

Alidokeza kuwa vile vile ni kisa kimaoja cha kifo kutokana na ugonjwa huu ambacho kilitokea mnamo 11, Oktoba 2024 kutoka kwa mgonjwa mabye alikuwa na maambukizi na kupona na kisha baadae akafa.

Aidha waziri huyo alisema kuwa wamweka mipango kabambe hili kuhakikisha kwamba wamefanya vipimo kwa viingilio vyote vya Kenya kwa nchi za kigeni.Vile vile alisema kuwa wasafiri takriban 1,362,657 wameweza kufanyiwa vipimo kwa viingilio 26 baada ya kukurupuka kwa ugonjwa huu.

Vinginevyo alisema kuwa mahabara ya kitaifa inazidi NPHL inaendelea na juhudi za kufanya vipimo zaidi akisema vipima 244 zimefanyika huku 14 zikiwa na maambukizi na 3 kufika sasa zinazidi kuchunguzwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved