
Mkenya aliyefichua mpango wa serikali kukodisha uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nelson Amenya sasa anadai kuwa maafisa wa
polisi wa kitengo cha upelelezi DCI wanamtafuta.
Amenya amesema kuwa maafisa hao aliowataja kama Subaru Gang, walifikia nyumabni kwao na kwa karakana ya rafiki wake siku chache zilizopita kwa madai ya kutafuta gari lililodaiwa kuibwa.
Kwa mujibu wa Amenya, maafisa hao wa polisi walifika nyumbani kwa wazazi wake wakidai kuwa walipata taarifa ya gari lililoibiwa kuwa limeegeshwa katika boma lao. Aliongeza kusema kuwa polisi hao walifanya msako hadi kwa paa ya ghorofa kisha wakaondoka.
Baada ya kuondoka nyumbani kwa wazazi wake, Amenya amesema kuwa mafisa hao walienda kwa karakana ya rafiki yake ambapo walidai kuwa walikuwa wanatafuta gari aina ya Mercedes muundo wa kisasa lililokisiwa kuwa sehemu hiyo.
“Baadaye, walienda kwa karakana ya rafiki mara hiyo wakisema walikuwa
wanatafuta gari aina ya Mercedes muundo mpya lililoibwa wa walikuwa na habari
lilikuwa pale.” Aliandika Amenya kwenye ukurasa wa X.
Aidha, Amenya amewatahadharisha maafisa hao kuwa anawajua na ikiwa kitu chochote kitawafanyikia watu walio karibu naye dunia nzima itafahamu majina yao.
Hata hivyo, amekashifu idara ya DCI kwa madai ya kutumia rasilimali za thamani kumlenga mkenya asiye na madhara kwa sababu ya kufichua siri ya mkataba baina ya Adani na JKIA.
Ameitaka idara hiyo badala yake kutumia
rasilimali hizo kupigana na mauaji ya wanawake yaliyokithiri na uhalifu pamoja
na ufisadi katika sekta za umma
