Mwakilishi wa kike wa kaunti ya Nairobi Esther Muthoni Passaris ameibua wasiwasi kuhusu unyanyasaji wa mtandaoni na wa kijinsia na baadhi ya vijana wa Kenya.
Wakati akizungumza katika hafla ya
hivi majuzi, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 60 alifichua kuwa baadhi ya vijana
wamekuwa wakimtumia picha za sehemu za siri tangu nambari yake ilipovujishwa
kwenye mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.
Passaris alitaja kitendo hicho kuwa ni ukosefu wa heshima na kuwataka wakome huku akieleza kwamba amehitimu kuwa mama kwa wale wanaomtumia picha hizo za utupu.
“Vijana, tafadhali. Sijui ni nini imetendeka na vijana wetu. Na tutakuwa na mpango wa kuwawezesha vijana ili tuzungumze vizuri. Kwa sababu, mimi nimeona ata mimi kama mheshimiwa, saa wengine vijana wananikosea heshima,” Esther Passaris alilalamika.
Aliendelea,“Unajua ile wakati niliweka namba yangu kwenye mtandao, wakaanza kusalimia kila mtu, wamenitumia mapicha ya vitu ambavyo ata sijui wanafikiria nini hiyo kitu, lazima niiangalie. Wengine wananiambia wako na ma-inches, sasa mimi najiuliza kama Watoto wangu, Mimi niko na miaka sitini, alafu unaniambie uko na inches, alafu unatoa suruali, unachukua picha, ata haijasimama, unanitumia. Unaniambie nifanye nini na hiyo kitu? Sasa unataka nifanyeje? au hata labda sio yako, umechukua picha kwa mtandao, kwa sababu hiyo huwezi piga picha, kwa sababu ukipiga picha haionekani.”
Mwanasiasa huyo ambaye alipigiwa
kura kwa tikiti ya chama cha ODM aliwataka vijana hao kuwa na heshima huku akiwaonya kuwa Mungu aliye mbinguni anatazama matendo yao.
Nambari ya simu ya Passaris ni miongoni mwa nambari ambazo zilivunjishwa kwenye mitandao ya kijamii wakati wa maandamano ya vijana nchini kote miezi michache iliyopita.
Vijana kwenye mitandao ya kijamii walivujisha namba za wanasiasa mbalimbali ambao walikuwa na hasira nao na kuwataka wenzao ‘kuwasalimia’.