Aliyekuwa Mwakilishi wa kike wa Kaunti ya Laikipia Catherine Waruguru mnamo Alhamisi , Novemba 28, alisimulia masaibu yake wakati wa kujifungua.
Mama huyo wa watoto watatu alikuwa mmoja wa wanasiasa wageni wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuripoti visa vya dhulma wakati wa uzazi (OBV) katika kituo cha Kenya Women and Children’s Wellness Center, eneo la Roysambu, Nairobi.
Waruguru alizungumza kuhusu jinsi alivyoogopa kuzaa tena baada ya yale aliyoshuhudia wakati wa kujifungua mtoto wake wa kwanza.
“Matukio yangu ya kwanza katika Hospitali Kuu ya Nanyuki haikuwa bora zaidi. Nahitaji kukiri, nilikimbia nikapotea zaidi ya miaka kumi. Sikuzaa tena kwa miaka kumi,” Waruguru alisema.
Mbunge
huyo wa zamani alikiri hayo wakati alipokuwa akitetea kuwepo kwa mazingira bora
na ya starehe wakati wanawake wanapojifungua kwa wanawake.
"Tunahitaji kuingia kliniki kwa ajili ya huduma za kabla ya kuzaa, kutunza ujauzito, kuingia katika wodi za uzazi na hata baada ya kujifungua kufanywa starehe na kwa heshima ambayo itamfanya mwanamke yeyote wa Kenya kujisikia kuheshimiwa nyumbani na nje ya nchi," alisema.
Waiguru alitetea usawa katika suala la mazingira ya huduma za afya kwa wanawake katika viwango vyote vya kiuchumi nchini.
Pia alitoa wito kwa Huduma mpya ya Bima ya Afya ,Taifa Care, ifanywe kuwa na ufanisi na kuhudumia Wakenya wote bila ubaguzi au kunyanyaswa.
"Ombi letu ni mwanamume au mwanamke yeyote wa Kenya anaweza kuingia katika kituo na kutibiwa bila kunyanyaswa au kuchukuliwa huku na huko," alisema.
Waruguru alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliokuwepo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Simu cha OBV katika eneo la Roysambu mnamo Novemba 28.
Wanasiasa wengine waliokuwepo ni pamoja na Mbunge wa Githunguri Gathoni Wamuchomba ambaye ni mwanzilishi wa Call Centre, mwakilishi wa Wanawake wa Kirinyaga Njeri Maina, mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi Esther Passsaris, Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, na mbunge wa kuteuliwa Teresia Wanjiru Mwangi.
Uzinduzi wa kituo hiki cha simu ni hatua muhimu katika kuhakikisha wanawake wanapata usaidizi, matunzo wanayostahili.
Wanawake sasa wanaweza kuripoti visa vya Dhulma wakati wa Kujifungua kwa nambari ya bila malipo 0111055181.