logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais William Ruto aungana na familia ya Lenny Kivuti kuomboleza kifo cha mwana wa seneta huyo wa zamani

Mwanawe Lenny Kivuti, Eric Mutugi aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya MP Shah

image
na Brandon Asiema

Habari23 December 2024 - 15:28

Muhtasari


  • Lenny Kivuti alikuwa seneta wa kaunti ya Embu kati ya mwaka 2013 na 2027.
  • Kwa mujibu wa Kivuti, Mutigi aliga baada ya kuugua kwa muda mfupi.


Rais William Ruto amejumuika na viongozi wengine katika kufariji familia ya aliyekuwa Seneta wa Embu, Lenny Kivuti, kufuatia kifo cha mwanawe, Eric Mutugi.

Katika taarifa yale iliyotolewa Jumatatu Disemba 23, rais Ruto alisema kuwa nyota ya Mutugi imezima mapema huku ahadi alizokuwa nazo zikikzimwa.

Kiongozi huyo wa taifa aliendelea kusema kuwa anaiombea familia ya Kivuti wakati huu wa kipindi kigumu cha maombolezo wanapokabiliana na msiba wa mtoto wao.

Vile vile kwenye ujumbe wake kupitia anwani ya X, rais pia aliomba faraja ya Mungu kwa familia na marafiki wa Kivuti.

“Naungana na familia ya Mheshimiwa Lenny Kivuti katika maombolezo ya msiba wa mwanawe mpendwa, Eric Mutugi. Ninaiombea familia ya Kivuti katika kipindi hiki kigumu sana. Nuru na ahadi ya Eric imechukuliwa hivi karibuni, Mungu awape familia na marafiki nguvu, faraja na amani,” Ruto alisema.

Lenny Kivuti alihudumu kama Seneta wa kwanza wa kaunti ya  Embu kuanzia 2013 hadi 2017. Kabla ya kuwa seneta Kivuti awali alihudumu kama mbunge wa Siakago.

Seneta huyo wa zamani alifichua kuwa mwanawe aliaga dunia katika hospitali ya MP Shah baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved