Polisi wa kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevywa katika kaunti ya Mombasa wanamzuilikwa mshukiwa mmoja anayedaiwa kuhusika katika ulanguzi wa mihadarati.
Mshukiwa huyo amabye alikamatwa katuika barabara kuu ya Nairobi – Mombasa mnamo Jumatano, alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Axio katika eneo la Jomvu.
Msako wa polisi kwenye gari lake ulibaini upatikanaji wa misokoto ya bangi iliyokuwa imefichwa kwenye buti ya gari hiyo. Kwa mujibu wa idara ya upelelezi kwenye ujumbe wake kwa anwani yake ya X, imesema kuwa walanguzi wa mihadarati wanajaribu kutumia mbinu mbali mbali ya kusafirisha dawa za kulevya.
Katika kisa kingine kwenye kaunti hiyo ya Mombasa, mshukiwa mwingine alifanikiwa kutoroka baada ya maafisa wa usalama kufanya msako dhidi ya mihadarati katika maeneo ya karibu na shule ya msingi ya Kiembeni.
Kwenye msako huo, maafisa wa polisi kutoka kituo cha Kiembeni walifanikiwa kupata gunia sita za bangi.Hata hivyo msako wa kumtafuta mshukiwa huyo unaendeshwa.
Hata hivyo mshukiwa wa kwanza aliyekamatwa katika eneo la
Jomvu, abnnazuiliwa na polisi katika kituo cha polisi cha Jomvu pamoja na
mihadarati aliyopatikana nayo ambapo atafikishwa mahakamani baadaye kujibu
mashtaka atayoshtakiwa nayo.